Wednesday, 27 May 2015

Russia yafungua soko lake kwa bidhaa za Iran

 http://kiswahili.irib.ir/media/k2/items/cache/0cd47ce9e034bc0abdc12960d91e8dd2_XL.jpg
Serikali ya Russia imeyaruhumu makampuni sita ya Kiirani kuingiza bidhaa zake za maziwa na chakula katika soko la nchi hiyo.
Katibu wa masuala ya habari wa idara ya masuala ya kusimamia ubora wa bidhaa za chakula Russia, Yulia Melano amesema kuwa, wameyaruhusu makampuni sita ya Iran kupeleka bidhaa za vyakula na mashirika manne kupeleka bidhaa za maziwa na makampuni mawili kuingiza bidhaa za jamii ya ndege ndani ya soko la Russia.
Russia imezipiga marufuku nchi za Ulaya, Marekani, Canada na Australia kuingiza matunda, mbonga mboga na samaki katika soko la nchi hiyo baada ya kuharibika mno uhusiano wa Russia na nchi za Magharibi huku Moscow ikizituhumu nchi za Magharibi kuingilia masuala yake ya ndani.
Hivi sasa Russia inatafuta marafiki wapya wa kibiashara baada ya kukatishwa tamaa na miamala ya kibeberu ya nchi za Magharibi.

No comments:

Post a Comment