WAZEE maarufu mkoani Rukwa, wakiongozwa na Mwanasiasa
mkongwe Dk.
Chrisant Mzindakaya wameanza kusaka suluhu ya kile kinachodaiwa ni
mgogoro baina ya waandshi wa habari na mkuu wa mkoa wa Rukwa Stella
Manyanya.
Dk. Mzindakaya aliambatana mzee Zeno Nkoswe ambaye ni mwenyekiti wa
Chadema mkoa wa Rukwa na mfanyabiashara maarufu Anyosisye Kiluswa
ambaye ni mlezi mstaafu wa Klabu ya waandishi wa mkoa huo.
Katika kikao hicho baina yao na uongozi wa Klabu ya waandishi wa
habari mkoa mkoa huo (RKPC) jana nyakati za saa moja jioni katika
hoteli ya Kalambo iliyopo mjini hapa ulilenga kutafuta suluhu mgogoro
huo ulisababisha waandishi kugoma kuandika na kutaangaza taarifa za
mkuu mkoa huo na Katibu tawala wake Salum Chima.
Kwa mujibu wa Dk. Mzindakaya alisema lengo wao kukutana na uongozi wa
Klabu ya waandishi wa habari mkoa huo ni kuanza harakati za kutafuta
suluhu ya mgogoro kwa manufaa ya maendeleo ya mkoa wa Rukwa.
"Sisi tumeona kuna tatizo hapa sasa hatuwezi kukaa kimya.......tumeona
tuchukue jukumu la kutafuta suluhu la ya kudumu kuhusu mgogoro kati
yenu na mkuu wa mkoa lengo tunataka muwe na mahusiano mazuri ya kikazi
na kibinadamu, tunajua kila binadamu hana mapungufu yake lakini
tutangulize maslahi mbele ya mkoa" alisema
Naye Mwenyekiti wa Chadema mkoa huo, Mzee Nkoswe alisema kuwa ni wazi
kwamba waandishi wa habari wamechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya
mkoa huo hivyo jitihada zao zinapaswa kutambuliwa na viongozi wa ngazi
zote na si kubezwa kama ambavyo baadhi ya watu wanavyofanya.
"Leo mkoa unafunguka kiuchumi, tuna miundombinu ya uhakika kama vile
barabara hii ni sehemu ya mchango wa waandishi wa habari wa mkoa huu,
na ieleweke kuwa bila waandishi wa habari hakuna maendeleo endelevu
popote pale" alisema Kiluswa.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Peti Siyame alisema kuwa
waandishi wa habari walichokifanya ni kutekeleza maagizo ya kikao cha
kamati ya utendaji cha Klabu hiyo iliyo kisheria kama taasisi huru
baada ya kuona mchango wao kwa maendeleo ya mkoa unapuuzwa.
Uongozi wa Klabu hiyo kupitia kikao chake cha Septemba 28 mwaka huu,
uligomea kwa muda usiojulikana kuandika na kutangaza taarifa zozote
zinazomhusu Mkuu wa Mkoa huo (Manyanya) kwa madai ya kutoa kauli za
kuwadhalilisha dhidi waandishi wa habari wa mkoa huo hadi hapo
atakapowaomba radhi.

No comments:
Post a Comment