Thursday, 19 December 2013
WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU WAFIKIA 6872 RUKWA.
BAADHI ya wakazi wa Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa, wametaka
uongozi wa Manispaa hiyo kuchuka hatua za makusudi kudhibiti tatizo la
ongezeko la watoto wa mitaa ambao wamekuwa kero kwa wananchi wa mji
huo.
Kwa mujibu wa afisa maendeleo ya jamii Manispaa ya Sumbawanga, James
Biseko Manispaa hiyo ina watoto wa mitaani 6872 ambapo kati ya hao
3268 ni wavulana na wasichana ni 3604.
Mmoja wa wananchi hao, Peter Mtuka alisema kuwa ongezeko la watoto wa
mitaani kubwa hivyo ipo haja sasa uongozi wa manispaa hiyo kuchukua
hatua za makusudi kudhibiti hali hiyo ambayo imekuwa ikisababisha kero
kwa wananchi.
"Hawa watoto ni kero sana maana wamekuwa wakitumia hadi silaha kutaka
pesa kwa watu...... kero inakuwa pale wanapowaomba pesa wakina dada na
wakina mama maana wakikataa hawana pesa wanawachanja na nyembe kitu
ambacho si sahihi" alisema Mtuka.
Uchunguzi wa mwandishi wa habari hizi mjini Sumbawanga, umebaini kuwa
watoto wengi wamekuwa omba omba kwa kufikiri ni njia rahisi ya
kuendesha maisha yao baada ya kutoroka kwenye familia zao kutokana na
sababu mbalimbali zikiwemo za kipato duni cha familia, malezi ya
wazazi wa kambo na tamaa.
Aidha, Biseko alisema kuwa moja ya mikakati ya Manispaa hiyo katika
kudhibiti hali hiyo ni pamoja na kushirikiana na asasi wadau wa
maendeleo ambapo kwa sasa Shirika la Pact - Tanzania lintekeleza
mradi uitwao pamoja tuwalee.
Alisema kuwa mradi huo unaolenga kumtaka mwana jamii asiwe tegemezi
katika kutunza na kusaidia watoto hao, hivyo wameanza kuwajengea uwezo
kuanzia ngazi ya kamati za mitaa na kata.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment