WATU watano
wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha za moto
aina ya SMG wamevamia kijiji cha Katisunga Wilaya ya Mlele
Mkoani Katavi na kuwapora wananchi vitu mbalimbali vya thamani zikiwemo fedha
taslimu Sh 740,000.
Kwa mujibu wa
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari, tukio hilo
lilitokea juzi saa 2:30 usiku katika kijiji hicho, ambapo majambazi hao
ambao walikuwa na bunduki aina ya Smg walifika kijijini hapo na
kuwavamia wananchi wa kijiji hicho waliokuwa wafanyabiashara wa
vibanda vya kuuza vocha na kutowa huduma ya Mpesa baada
ya kuwatisha kwa kufyatua risasi hewani.
Alisema kuwa
baada majambazi waliendesha operesheni hiyo kwa takribani saa moja ambapo
walifanikiwa kupora kiasi hicho cha fedha kutoka kwa watu waliokuwa wakitoa
huduma ya M Pesa na kuchukua na simu tatu zenye thamani ya Sh 450,000.
Kwa mujibu wa
Kamanda huyo wa polisi, mtu
mmoja aitwaye Justine Mkolwa
21 mkazi wa mtaa wa Makanyagio mjini Mpanda Dereva wa
gari aina ya Totota Hiluxe lenye namba za usajiri T800
ARN amekamatwa na anahojiwa kuhusiana na tukio hilo.
Hata hivyo
polisi bado inaendelea na uchunguzi kuhusu ilikuwabaini wale wote waliohusika
ili vyombo vya dola viweze kuwachukulia hatua za kisheria.
No comments:
Post a Comment