Na Walter Mguluchuma
Katavi
MHAKAMA ya Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi imemuhukumu mganga mkuu wa Zahanati ya Kasekese Wilaya ya Tanganyika Martin Mwashamba (27)kifungo cha miaka 30 jela baada ya kumtia hatiani kwa kosa la mbaka na kumpa mimba wanafunzi wa dasasa la sita wa shule ya Msingi Kasekese mwenye umri wa miaka 15 jina lake limehifadhiwa.
Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu mkazi wa Mahakama ya Wilaya hiyo Odira Amwol baada ya Mahakama kuridhika na ushahidi uliotolewa Mahakamani hapo na upande wa mashitaka.
Awali katika kesi hiyo mwendesha mashtaka Mwanasheria wa Serikali wa Mkoa wa Katavi Gregoli Mhagwa alidai Mahakamani hapo kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo siku ya Julai 2 mwaka jana Kijijini hapo.
Alieleza Mahakamani hapo siku hiyo ya tukio mshitakiwa alimbaka mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la sita wa shule ya Msingi Kasekese mwenye umri wa miaka 15 huku akijua kufanya hivyo ni kosa.
Upande wa mashitaka katika kaesi hiyo uliongozwa na mwanasheria Mhagwa ulikuwa na mashahidi watano na miuongoni mwao alikuw ni mwanafunzi aliyetendewa kitendo hicho na mshitakiwa kwa upande wake wa utetezi alikuwa na mashahidi watatu .
Hakimu Amwol kabla ya kusoma hukumu hiyo aliiambia Mahakama kuwa kutokana na ushahidi uliotolewa Mahakamani hapo na upande wa mashitaka Mahakama pasipo kuacha shaka lolote imemtia mshitakiwa hatiani kwa mujibu wa kifungu cha sheria 130 kifungu kidogo cha kwanza na chapili na kifungu cha sheria namba 131 kidogo cha kwanza cha kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2002.
Baada ya kutoa maelezo hayo Hakimu alitaka mshitakiwa kama anayosababu yoyote ya msingi ya kuishawishi mahakama ili impunguzie adhabu basi anapewa nasafi hiyo kabla ya kusomewa hukumu.
Mshitakiwa Mwashamba Katika utetezi wake aliiomba Mahakama impunguzie adhabu kwa kile alichodai kuwa yeye anafamilia inayomtegemea na pia ana wadogo zake watatu ambao anawasomesha yeye .
Hata hivyo utetezi huo ulipingwa vikali na mwendesha mashitaka mwanasheria wa Serikali Gregoli Mhagwa ambae aliiomba Mahakama itoe adhabu kali ili iwefundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo .
Hakimu Amwol baada ya kusiliza pande hizo mbili za mashitaka na utetezi aliiambia Mahakama kuwa mahakama imetowa adhabu ya kumuhukumu mshitakiwa Tabibu wa Zahanati ya Kasekese Martin Mwashamba kutumikia jela kifungo cha miaka 30 kwa kosa la kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 16.
MWISHO
No comments:
Post a Comment