Na Gurian Adolf
Nkasi
MWANAFUNZI wa darasa la pili shule ya msingi Kipundu James Kandege (8) amefariki dunia baada ya kupigwa radi juzi jioni akiwa nyumbani kwao na wenzake.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na afisa mtendaji wa kijiji cha Mabatini kata ya Namanyere Ibrahimu Adriano alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi jioni majira ya saa 10 alipokuwa ameketi nyumbani na wenzie walipokuwa wakila chakula cha mchana.
Alisema kuwa marehemu akiwa na wenzie sambamba na wazazi wake wakila chakula katika kitongoji cha Katowa kijiji cha Mabatini walipigwa na radi wakiwa ndani ya nyumba yao na mwanafunzi huyo alifariki dunia papo hapo huku wengine wakisalimika.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kipundu Josephat Laban athibitisha kutokea kwa kifo cha mwanafunzi huyo ambapo alisema kuwa shule hiyo iliwaruhusu Wanafunzi wote walishiriki katika msiba huo sambamba na mazishi huku akidai kuwa shule imempoteza mtu muhimu.
Diwani wa kata ya Namanyere Evarist Mwanisawa alisema kuwa Mwanafunzi huyo alikua ni mkazi wa kitongoiji cha Katowa na ndiko alikokutwa na mauti na kuwa mazishi ya mtoto huyo yamefanyika katika kijiji cha Lunyala.
Mkuu wa wilaya Nkasi Said Mtanda amekiri kutokea kwa kifo hicho na kuwa na kuwa wakati radi hiyo ikipiga Mwanafunzi huyo alikua pamoja na watoto wenzie na wazazi wake wote wawili wakila chakula ambapo katika hao hakuna mwingine aliyepata madhara yoyote .
Alisema kuwa serikali kupitia idara ya elimu msingi wilayani humo imeshiriki katika mazishi ya mwanafunzi huyo licha ya kudai kuwa watu wengi walishikwa na simanzi kutokana na tukio hilo.
Katika siku za hivi karibuni wilaya Nkasi kumekuwa na matukio ya mara kwa mara ya watu kupiga radi na kusababisha vifo au mifugo kufa kiasi cha wananchi kuishi kwa hofu huku wakiwa hawajui nini cha kufanya.
mwisho
No comments:
Post a Comment