Na Gurian Adolf
Katavi
MKAZIwa kijiji cha Ntumba kilichpo wilayani Tanganyika katika mkoa wa Katavi, Charles Sabuni (37) amepwa viboko 30 hadharani baada ya kushikwa ugoni na mke wa jirani yake Ntema Mwiwela, juzi usiku wa manane kijijini hapo.
Kwa mujibu wa Taarifa kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa adhabu hiyo alipewa mgoni huyo ili iwefundisho kwake na kwa wanaume wengine wenye tabia kama hiyo.
Akisimulia tukio hilo mwenyekiti wa Kitongoji cha Ntumba Samwel Mbuya alisema lilitokea saa tisa usiku, juzi nyumbani kwa Mwiwela ambaye anaishi jirani na Sabuni.
Akifafanua alisema kuwa mchana wa siku hiyo ya tukio hilo Mwiwela alimuaga mkewe kuwa ana safiri ambapo alirejea nyumbani kwake ghfla usiku wa manane na kumkuta Sabuni akiwa amelala chumbani kwake.
“Mwenye mke alimthibiti mgoni wake huyo asitoroke huku akimwamuru apige mayowe huku akisema anaomba msaada kwani amefumaniwa na mke wa mtu ….. kele hizo ziliwaamsha wanakijiji wenzake ambao walikimbilia eneo la tukio na walipigwa na kutwaa kumkuta Sabuni akiwa chumbani chini ya ulinzi wa Mwiwela “ alieleza.
Alieleza kuwa wananchi hao walielezwa na Mwiwela kitendo alichofanyiwa na jirani yake Sabuni ambapo walipandwa na hasira na kuamuru aendelee kuwa chini ya ulinzi hadi kutakapopambazuka .
Inadaiwa kulipokucha wananchi hao wenye hasira walimuaru mwenzao huyo apewe adhabu kali ya kucharazwa viboko hadharani ili iwe fundisho kwake na kwa wanaume wengine wenye tabia kama hiyo
Hata hivyo Sabuni alinusurika baada ya viongozi wa kitongoji wakiongozwa na mwenyekiti Mbuya na kuwazuia wasimcharaze viboko hadharani kwa kuwa watakuwa wamekiuka haki za binadamu .
Ndipo kilipoitishwa kikao cha dharura kikiwajumuisha viongozi wa serikali wa kitongoji hicho, wazee pamoja na Mwiwela na ‘mgoni wake ambapo baada ya majadiliano marefu Sabuni alikubali kumlipa faini faini ya kiasi cha Shilingi 800,000/- ikiwa ni fedha alizotoa mahali wakati muoa mke wake .
Kwa mujibu wa Mbuya mara tu Mwiwela alipokabidhiwa kiasi hicho cha fedha hapo hapo alimkabidhi mke wake kwa Sabuni akidai kuwa hawezi kuendelea kuishi naye kwa sababu sio muaminifu.
Mwisho
No comments:
Post a Comment