Na Gurian Adolf
Katavi.
Jeshi la Polisi mkoani Katavi linamshikilia mkazi wa Kijiji cha Songambele Kata ya Sibwesa Tarafa ya Karema Wilaya ya Tanganyika jina lake limehifadhiwa(45) kwa tuhuma za kumuua mke wake(31) kwa sababu ya wivu wa kimapenzi na kisha mzika huku mtoto wake mwenye umri wa miaka tisa akishuhudia tukio.
Kamanda wa Jeshi la Polisi wa mkoa wa Katavi Damas Nyanda alisema tukio la kupatikana kwa mwili wa marehemu huyo lilitokea juzi majira ya saa 6;00 mchana katika Kijiji hicho.
Alisema kuwa marehemu aliuawa na mumewe huyo siku ya hapo januari 15 kwa kupigwa na mumewe kwa kutumia silaha zajadi ambazo ni fimbo na mpini wa jembe baada ya kumtuhumu kuwa anamahusiano wa kimapenzi na wanaume wengine Kijijini hapo.
Kamanda Nyanda alisema kuwa wakati mtuhumiwa huyo akitenda kosa hilo ambalo lilishuhudiwa na mtoto wake wa kiume hadi baba yake alivyo muuawa mama yake na kisha kushimba shimo na kumfukia ardhini.
Baada ya kufanya mauaji hayo na kuzika mwili huo mtuhumiwa alirejea nyumbani kwake na kuendendelea na shughuli zake kama kawaida na alimtishia mtoto wake huyo mdogo na kumwambia asimwambie mtu yeyote.
Majirani waliokuwa wakimfahamu marehemu baada ya kuona haonekani Kijijini hapo walianza kumuuliza mtuhumiwa mahali alipo mkewe naye alikuwa akiwajibu kuwa mkewe amesafiri kwenda kwao kusalimia.
Kamanda huyo wa polisi alisema kuwa Jeshi la polisi lilipata taarifa ya mauaji ya mama huyo hapo machi 15 na ndipo lilipoanza uchunguzi wa tukio hilo.
Alileza baada ya kufanya uchunguzi wa kina ndipo juzi waliweza kumtia mbaroni mtuhumiwa na baada ya mahojiano alikiri kufanya mauaji hayo kwa kile alichodai kuwa alikasirishwa na tabia ya mke wake ya kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanaume wengine kijijini hapo na aliwaeleza polisi kuwa yuko tayari kwenda kuwaonyesha alipofukia mwili wa mke wake baada ya kufanya mauaji.
Baada ya mahojiano hayo hapo juzi majira ya saa 6;00 mchana polisi walifika kwenye eneo ambalo mtuhumiwa alikuwa amemfukia marehemu mkewe na baada ya kufukua eneo hilo walikuta mwili na kuutambua kuwa ni mwili wa mwanamke huyo na kisha kuutoa katika eneo hilo.
Kamanda Nyanda alisema kuwa mwili wa marehemu baada ya kufukuliwa ulichukuliwa na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika Manispaa ya Mpanda.
Mtuhumiwa anaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi na mara baada ya upelelezi kukamilika anatarajiwa kufikishwa mahakamani ili akajibu tuhuma zinazo mkabili.
Mwisho
No comments:
Post a Comment