Na Gurian Adolf
Katavi
Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya rais Tamisemi George Kakunda ameuagiza uongozi wa Serikali ya wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi kuwafukuza kazi walimu walio na mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi wao.
Naibu waziri huyo alitoa agizo hilo jana wakati akizungumza na Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Nsimbo pamoja na watumishi wa halmashauri hiyo katika ukumbi wa mikuto wa halmashauri hiyo.
Kabla ya kutoa agizo hilo Diwani wa Kata ya Katumba Seneta Baraka alimweleza Naibu Waziri Kakunda kuwa yeye kama Diwani maisha yake yako hatarini kutokana na kuwafatiliwa na walimu wanaofanya mapenzi na wanafunzi wao.
Alisema kumekuwa na tabia sugu kwa baadhi ya walimu wa Shule mbili za Sekondari katika Makazi ya Wakimbizi ya Katumba ya kufanya mapenzi na wanafunzi wao na wengine kuwaoa kwa madai kuwa walimu kufanya mapenzi na wanafunzi wao ndio ruzuku yao.
Diwani huyo alisema amekuwa amekuwa akipata ushirikiano mdogo kutoka kwa uongozi w wilaya licha yeye kutoa taarifa za tabia hiyo lakini hakuna hatua zilizochukuliwa licha ya kuwepo kwa ushahidi na matokeo yake yeye ndio amekua akitishiwa maisha.
Diwani Seneta alizitaja shule za Sekondari ambazo baadhi ya walimu wake wanatabia ya kufanya ngono na wanafunzi wao kwa kisingizio cha kuwa ni ruzuku kwao kuwa ni Katumba Sekondari pamoja na Kenswa Sekondari.
Seneta alilifafanua kuwa yupo mwalimu mmoja ambaye aliamua kumwoa kabisa mwanafunzi wake na swala hilo alishalizungumza kwenye baraza la madiwani lakini hakuna hatua zilizochukuliwa na badala yake baadhi ya madiwani wenzake wamekuwa ndio wakwanza kuwafikishia taarifa walimu kuwa yeye ndio anae shupalia jambo hilo.
Alisema kuwa mwalimu mmoja baada ya penzi kukomaa na mwanafunzi wake aliamua kmuoa kabisa na wanaishi nae na aliamua kupeleka mahali kwa wazazi wake hata hivyo mama mzazi wa mwanafunzi huyo alikataa kupokea pesa za mwalimu huyo.
Alimwomba waziri Kakunda amsaidie ili aweze kupatiwa ulinzi kwani vitisho anavyo pata vinahatarisha maisha yake na ndio maana siku hizi amepunguza hata kutembelea kwenye maeneo ya starehe kwa kuhofia maisha yake.
Mara baada ya kupokea maelezo hayo naibu Waziri aliungiza uongozi wa Serikali ya wilaya ya Mpanda kuhakikisha inawachukulia hatua walimu hao maramoja ikiwemo kuwafukuza kazi
Alisema sheria inakaza kufanya mapenzi na mtoto mwenye umri chini ya miaka 18 hivyo wanaofanya hivyo watambue kuwa wanafanya makosa na wala hakuna kusingizia kuwa walikubaliana .
Kakunda alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha mtoto anasoma kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne hivyo aliwaonya wanaowaozesha wanafunzi wakae chonjo kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria.
Alizitaka kamati za ulinzi na usalama za Kata nchi nzima zishirikiane kufanya kazi ya kuhakikisha zinadhibiti mimba za wanafunzi kwenye kata zao.
Kwaupande wake ofisa elimu Sekondari ya halmashauri ya wilaya ya Nsimbo Said Malamba alisema kuwa swala hilo tayari amekwisha anza kulishughulikia.
Alisema tayari walmu wawili wa shule ya Sekondari ya Katumba na mmoja wa Seokndari ya Kenswa walisha andikiwa barua na tume ya utumishi ya kujieleza kutoka na tuhuma hizo na baada ya kujieleza tayari mwalimu Mmoja wa Shule ya msingi Katumba mwalimu ambaye ni mwalimu Fransis Manyala amechukuliwa hatua na walimu wawili hawakupatikana na hatia.
Alisema mwalimu huyo aliyepatikana na hatia tume ya utumishi ya wilaya ya Mpanda amekata rufaa kwenye tume ya utumishi Taifa baada ya kutoridhika na maamuzi ya kusimamishwa kwake kazi.
Mwisho
No comments:
Post a Comment