Sumbawanga
MKUU wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo amewaambia wazazi mkoani humo kuwa huduma mbovu wanazopata kutoka kwa watumiashi wa umma zinatokana na malezi mabaya ya wazazi dhidi ya watoto wao.
Kauli hiyo aliitoa jana katika mji mdogo wa Laela wilayani Sumbawanga wakati akijibu malalamiko mbalimbali ya wananchi alipokuwa kwenye Siku yake ya pili ya ziara ya kikazi wilayani humo.
Alisema kuwa wananchi wamekuwa wakiwalalamikia watendaji wa serikali kwa kutoa huduma mbovu na majibu mabaya lakini wanasahau kuwa watendaji hao wanatoka kwao kwakua ni watoto wao hivyo hayo wanayofanya yanatokana na malezi mabaya tangu utotoni.
Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa miongoni mwa mambo ya msingi ni malezi ya mtoto tangu nyumbani kwani baadhi ya wazazi hawajali kuhusu malezi ya watoto wao ndio maana anapo kuja kuwa mtumishi wa umaa anakua mtu wa hovyo.
"wapo baadhi ya wananchi wanao lalamikia tabia mbaya ya watendaji wa serikali lakini wanasahau kuwa wao ndio wanao walea watendaji hao tangu wakiwa wadogo kwahiyo hata hayo wanayo tendewa yanatokana na malezi mabaya"alisema
Alisema ikiwa wanataka kupunguza malalamiko dhidi ya watendaji wa serikali nilazima wawalee watoto wao kwa kuzingatia maadili mema vinginevyo malalamiko hayataisha.
"utakuta mzazi anakwenda kilabuni kunywa pombe akiwa na mtoto mgongoni, akinywa anampa na mtoto anywe,sasa akiwa mtumishi mlevi mnailaumu serikali kuwa mtumishi wake ni mlevi wakati wazazi ndio chanzo cha ulevi wa mtumishi huyo.
Aliwaasa wazazi kuzingatia malezi bora ya watoto ili serikali iweze kupata watumishi wema,wasio penda rushwa,wenye nidhamu na wachapakazi ili jamii iache kulalamikia tabia mbaya za watumishi.
Naye mkuu wa wilaya ya Sumbawanga Dkt Khalfan Haule alimwagiza mkurugenzi wa halmashauri hiyo John Msemakweli kuwahamisha watendaji waliokaa katika vituo vya kazi kwa muda mrefu ili kuboresha utendaji.
Alisema baadhi ya watumishi wamekaa katika vituo vya kazi kwa muda mrefu hadi inafika wakati wanashindwa kutimiza wajibu wao kutokana na kuathiriwa na mazingira pamoja na mahusiano ya kidugu.
Hata hivyo mkurugenzi Msemakweli aliwaasa watendaji wa serikali kuwa heshimu wananchi kwani wanalipwa mishahara kutokana na kodi za wananchi hao ambao hawawatendei haki.
Awali katika mkutano huo wa hadhara wakazi wa mji mdogo wa Laela wilayani Sumbawanga mmoja wa wakazi aliwalalamikia watendaji wa afya kituo cha afya Laela kutokana na majibu mabaya kwa wagonjwa na kuwanyima huduma.
Kwaupande wake mwenyekiti wa halmashauri hiyo ya Sumbawanga Kalolo Ntila alisema kuwa uchunguzi utafinyika dhidi ya watumishi hao waidara ya afya na iwapo tuhuma hizo zitabainika kuwa nikweli baraza la madiwani litawashughulikia kwani halipo tayari Kuhamisha watumishi wabovu kwani hao ndio wanao wasababishia matatizo wakati wa uchaguzi.
Mwisho
No comments:
Post a Comment