Nkasi
SERIKALI wilayani Nkasi mkoani Rukwa imewaonya mafataki kuwaacha watoto wa kike wasome kwani wamekuwa wakikatiza ndoto zao kwa kuwapa mimba na hivyo kuwaharibia maisha.
Mkuu wa wilaya hiyo Said Mtanda aliyasema hayo jana wakati Akizindua mashindano ya mpira wa miguu yaliyo andaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Plan International kwa lengo la kupinga mimba za utotoni.
Alisema kuwa wapo baadhi ya wanaume wilayani humo wamekuwa wakiwaharibia maisha wanafunzi kwa kuwapa mimba hali inayowafanya wakatishe masomo na kushindwa kufikia ndoto zao.
Mtanda alisema serikali ya wilaya hiyo kamwa haitawavumilia wanaume hao wajiandae kuchukuliwa hatau kwakua haipo tayari kushuudia mtoto wa kike akikatiza masomo kwasababu ya kupata mimba.
"Mafataki wote waacheni watoto wa kike wasome wafikie ndoto zao ndipo ufuate taratibu kisha umuoe awe mke wako,lakini kamwe hatutakubari kuwaharibia maisha kwa kuwapa mimba".alisema
Alisema kuwa katika wilaya hiyo kumekuwa na mdondoko kwa watoto wa kike kwa kuacha masomo kwasababu ya ujauzito hivyo nilazima jamii nzima itambue kuwa hilo suala halikubaliki na litavaliwa njuga kuhakikisha linakwisha kabisa.
Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha mkuu wa wilaya hiyo mratibu wa Plan International wilayani Nkasi Nestory Frank alisema kuwa lengo la kuandaa mashindano hayo ni kuwakutanisha wazazi pamoja na vijana ili kufurahia michezo lakini pia kuwa kumbusha haki za mtoto wa kike ikiwemo fursa ya kupata elimu.
Alisema kuwa mradi huo unafadhiliwa na shirika la Plan International ambapo ulianza kutekelezwa Mwaka 2016 na utamalizika Mwaka 2019 na una tekelezwa katika kata za Mkwamba,Mtenga na Nkandasi wilayani humo.
Mwisho
No comments:
Post a Comment