Na Gurian Adolf
Sumbawanga
MBUNGE wa jimbo la Sumbawanga mjini ,mkoani Rukwa,Aesh Hilary amewaomba wakazi wa kata ya Sumbawanga Asilia kuhakikisha wanafanya kampeni za kistaarabu ili chama hicho kipate ushindi na kuendelea kumpa fursa rais John Magufuli ili awatumikie.
Ombi hilo aliltoa jana kwa wakazi wa kata hiyo wakati akizindua kampeni za chama cha Mapinduzi(CCM) kwa lengo la kuwania kata hiyo ambayo inafanya uchaguzi baada ya diwani wa awali kufariki dunia.
Alisema kuwa hivi sasa ni wakati wa kupiga kampeni za kistaarabu ili hata wasiokuwa wanachama wa chama hicho wavutiwe na kujiunga kwani hivi sasa ni wakati wa kurudisha wanachama walio hama na moja kati ya mikakati ni kupiga kampeni za kistaarabu ili chama hicho kipate ushindi.
Hilary alisema kuwa kata hiyo ilikuwa chini ya Chadema lakini imefika wakati waichukue kwakua wakazi wa kata hiyo wanavutiwa na utendaji kazi wa mwenyekiti wa CCM taifa, hivyo anaamini hawataweza kukinyima kura chama cha Mapinduzi kwani hivi sasa kimejikita kuwaletea maendelo.
''ndugu zangu wananchi wa kata ya Sumbawanga Asilia kilichopo mbele yetu ni ushindi,tupige kampeni za kistaarabu,hatuhitaji ubabe,tuhakikishe tunashinda,pia niwakati muafaka wa kuhakikisha wale wote waliokihama chama chetu wakati wa uchaguzi mkuu uliopita wanarudi,naamini wameona tunavyotekeleza ilani ya chama ninaamini watatupa ridhaa ili tuendelee na kazi nzuri'' alisema.
Alisema kuwa halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga imepiga hatua kubwa katika miradi ya maendeleo hasa katika suala la ujenzi wa barabara,huduma za maji safi,umeme afya na nyinginezo ni kwasababu ya ilani nzuri ya chama cha Mapinduzi hivyo basi ni wakati wa kukipa kura ili kishinde kata hiyo.
Kwaupande wake mgombea wa udiwani katika kata hiyo kupitia CCM, Cornel Kufumu aliwaomba wapiga kura wampe kura zote apate wa kishindo ili aweze kushinda aingie katika baraza la madiwani ashirikiane na waliopo katika kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Alisema kuwa pamoja na kwamba watamchagua yeye atahakikisha anawatumikia wananchi wote wa kata hiyo bila kujali itikadi za chama kwani maendendeleo hayana chama na yeye anachotaka kuona ni wananchi wanapata maendeleo.
Mwisho
No comments:
Post a Comment