Na Walter Mguluchuma
Katavi
Serikali imeingilia kati mgogoro wa muda mrefu baina ya wafugaji na uongozi wa pori la akiba la Rukwati lilopo mkoani Katavi,ambapo imeamuru wafugaji warejeshewe ng'ombe zaidi ya 600 walioingizwa kwaajili ya kuchungiwa ndani ya pori hilo.
Waziri wa mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina alitoa agizo hilo baada ya kubani mifugo hiyo inashikiliwa wakati hakuna hati yoyote inayowataka kuishikilia mifugo hiyo.
Uongozi wa pori la akiba la Rukwati uliwakamata ng'ombe 1,332 mwaka jana mali ya wafugaji watatu katika waishio katika bonde la ziwa Rukwa kwa kosa la kuchungia katika pori hilo la akiba.
Waziri Mpina alilazimika kufika kwenye pori hilo kwa lengo la kutatua mgogoro huo ulikuwa umedumu kwa muda mrefu na kujiaonea hali halisi ya mazingira ya mifugo hiyo ilikuwa ikiendelea kushikiliwa.
Alisema kuwa alishitushwa na taarifa iliyotolewa na Meneja wa pori hilo Pascal Mhina ambae alimweleza kuwa Wanashikilia ng'ombe 1,332 kwa zaidi ya mwaka mmoja na miezi tisa kati ya ngombe hao 692 wamekufa na wamebaki 640.
Hivyo aliwaagiza viongozi wa Serikali wa mkoani Katavi kuhakikisha mifugo hiyo wanaikabidhi kwawenyewe na kwa watumishi watakao bainika walisababisha uzembe wa vifo vya mifugo hiyo watashukuliwa hatua na mamlaka husika.
Alisema kulikua hakuna sababu ya msingi ya kuendelea kuishilikia mifugo hiyo baada ya wao kuwafungulia mashitaka watuhumiwa watatu kwa kuingiza mifugo kwenye pori hilo na katika kesi ya awali iliyosikilizwa katika mahakama ya wilaya ya Mpanda ilitowa hukumu na kuamuru mifugo hiyo itaifiswe iwe mali ya Serikali.
Alimtaka meneja wa pori la akiba amwoneshe hati yoyote inayowapa mamlaka ya kuendelea kuwashikilia ng'ombe hao wakati wafugaji walikuwa wanatuhumi baada ya hukumu ya mahakama ya wilaya ya Mpanda kutoa uamuzi wa kutaifisha mifugo watuhumiwa walikata rufaa mahakama kuu ya Sumbawangambayo ilitengua maamuzi ya mahama ya wilaya na iliamuru wafugaji watatu Shigela Mayunga,Charles Mtokambali na Kelenja Makuja warejeshewe mifugo yao pamoja na faini ya shilingi 500,000 walizokuwa wametozwa.
Waziri Mpina alisema amesikishwa na kitendo cha uongozi wa pori la akiba kuridhika kuona ng'ombe wote hao wamekufa kwa magonjwa na wao ndio walio sababisha hali hiyo.
Waziri huyo pia alitaka jua ni nikwanini mifugo hiyo iliendelee kuwa ndani ya pori hilo wakati eneo hilo ni maaluumu kwa wanyama wa porini wakati mifugo inasheria zake.
Meneja wa Pori la akiba Mhina alieleza kuwa waliendelea kuishikilia mifugo wakisubiri mahakama kuu ya kanda ya Sumbawanga itoe maamuzi kufuatia rufaa iliyokatwa na wafugaji hao.
Alisema waliendelea kuishikilia kwakua walipewa maelekezo na mwanasheria wa Serikali waendelee kuitunza mifugo hiyo kama sehemu ya kielelezo cha kesi hiyo.
Baada ya maamuzi hayo ya waziri, Katibu Mkuu wa Chama cha Wafugaji Tanzania Makoye Nkonosine aliiomba Serikali iwapatie mifugo ya wafugaji hao ambayo ilikuwa hai na ile ambayo imekufa wataendelea kudai.
Aidha alitaka kufahamishwa kwa kipindi chote hicho ni ndama wangapi waliozaliwa kwani taarifa iliyotolewa hapo ya ng'ombe 1,332 kwa kwa muda wote huo mifugo hiyo pia iliweza kuzaa.
Nae Afisa utafiti wa magonjwa ya mifugo wa Mikoa ya Katavi na Rukwa Protus Reshola alisema kuwa idadi hiyo ya ng'ombe waliokufa ni kubwa na imetokana na sababu mbalimbali kama ikiwemo ya watu walikuwa wakichunga mifugo hiyo sio wafugaji.
Pia alisema mifugo hiyo ilikufa kwakuwa ilikuwa haitibiwi homa ya mapafu na kwenye maeneo hayo kulikuwa hakuna josho pia kuchanganya ng'ombe kutoka katika maeneo tofauti.
Mwisho
No comments:
Post a Comment