Nkasi
SERIKALI wilayani Nkasi mkoani Rukwa imelazimika kuendesha zoezi la kura ya siri ili kuwabaini watu wanaowapa ujauzito wanafunzi baada ya wanafunzi 152 kuripotiwa kupata ujauzito katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.
Mkuu wa wilaya hiyo Said Mtanda aliongeza zoezi hilo baada ya kubaini idadi hiyo ya wanafunzi kupata ujauzito lakini hakuna mtu aliye kuhukumiwa kwa kosa la kumpa mimba mwanafunzi.
Akizungumza katika zoezi hilo mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa ameamua kufanya hivyo kutokana na taarifa kuwa wapo baadhi ya walimu na wananchi wengine ambao wamekuwa kinara katika vitendo vya kujihusisha na mapenzi na wanafunzi.
"haiwezekani suala hili likafumbiwa macho, lazima tuchukue hatua hata kwa kupiga kura ya siri mradi tuwabaini wanaojihusisha na mapenzi na wanafunzi kwani tusipo chukua hatua watatumalizia wanafunzi wakike kwakuwapa mimba"
Katika kura hiyo yasiri walimu watatu kutoka Shule ya Chala Sekondari ambapo kura nyingi ziliwaangukia wakituhumiwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi pamoja na wakazi wengine wa kijiji cha Chala ambapo zoezi hilo likianzia.
Kwaupande wake diwani wa kata hiyo Michael Mwanalinze alimuomba mkuu huyo wa wilaya kuendesha kura hiyo katika Kata zote za wilaya hiyo ili kuwakomesha wenyetabia za kuwa na mahusiano na wanafunzi.
Aliwasihi wanafunzi kuacha kuendekeza vitendo vya mapenzi badala yake wakazanie masomo kwani wakimaliza watafanya vitendo hivyo mpaka viwakinahi.
Mwisho
No comments:
Post a Comment