Na Gurian Adolf
Katavi
Mahakama ya wilaya ya Mpanda mkoani Katavi imemuhukumu Willson John(34) mkazi wa Kijiji cha Simbwesa wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi kutumikia jela kifungo cha maisha baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto (7)wakati akiwa anaoga bafuni.
Hukumu hiyo ilitolewa jana na hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya hiyo Chiganga Ntengwa baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka.
Kabla ya kusoma hukumu hiyo hakimu Ntengwa alisema mtu yoyote anaefanya kitendo kama alichofanya mshitakiwa huyo anakuwa amefanya kosa kinyume cha kifungu cha sheria namba 130 kifungu kidogo cha kwanza na 2E cha sheria namba 131 kidogo cha tatu cha kanuni ya adhabu.
Alieleza kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani na upande wa mashtaka uliotolewa na mashahidi sita akiwemo mtoto aliyebakwa ambapo mshitakiwa hakuwa na shahidi yoyote na mahakama imeridhika na ushahidi huo wa upande wa mashtaka.
Hakimu Ntengwa alisema kuwa miongoni mwa ushahidi uliomtia mshitakiwa hatiani ni ule uliotolewa na mtoto mwenyewe aliyefanyiwa kitendo hicho pia daktari aliyemfanyia uchunguzi na kuthibitishwa kuingiliwa kwa mtoto huyo kwenye sehemu zake za siri na kuharibiwa hali iliyomlazimu kumwanzishia dawa za kumkinga na maambuzi ya VVU.
Pia ushahidi mwingine ni wa mama mzazi wa mtoto huyo ambaye aliutoa mahakamani kuwa mtoto wake alibakwa.
Awali katika kesi hiyo mwanasheria wa Serikali Fravian Shiyo alidai mahakamani hapo kuwa mshitakiwa John alitenda kosa hilo Septemba 24 mwaka huu majira ya saa 2:30 usiku nyumbani kwao na mtoto huyo ambako mshitakiwa alikuwa amepanga chumba kwenye nyumba yao wazazi wa mtoto aliyembaka na wakati antenda kosa hilo wazazi wa mtoto huyo walikuwa wakiangalia mpira sebuleni kwenye TV.
Alieleza siku ya tukio hilo mtoto huyo alikua amechukua maji kwaajiri ya kuingia bafuni kuoga wakati alipokaribia kwenye mlango wa bafuni alimkuta mshitakiwa akiwa amesimama karibu na mlango wa kuingilia bafuni na ndipo mshitakiwa alipomtolea kauli na kusema wewe ingia tuu bafuni uoge na mie nakuja kupata haja ndogo humo humo.
Mwanasheria shiyo alisema wakati mtoto huyo akiwa anaendelea kuoga mshitakiwa Willson aliingia ndani ya bafu na kumziba mdomo iliasipige kelele mtoto huyo na kisha na kisha alianza kumbaka na alipomaliza alimwachia mtoto huyo na kumwambia kuwa endapo angemwambia mtu yeyote juu ya kitendo alichomfanyia atamuua.
Aliendelea kuieleza mahakama hiyo aliyebakwa awe mwoga na asiwaambie wazazi wake na aliingia ndani na kumwomba Mama yake ampatie maji ya kunawa hata hivyo mama yake alimkatalia kumpa maji kwa kile alichodai mbona ametoka kuoga muda si mrefu maji ya nini tena.
Ndipo mtoto huyo alipoingia ndani ya chumba alichokuwa akilala hata hivyo alishindwa kupata usingizi kutokana na maumivu yalivyozidi alimwagiza mtoto mwezake wa kike amwite mama yake na alipoingia chumbani alimkuta akiwa analilia huku godoro alilokua amelalia likiwa limelowa damu na ndipo alipomtaja mtuhumiwa kuwa ndio aliyembaka.
Kabla ya kusomewa hukumu mshitakiwa alipewa ya nafasi ya kujitetea kama anayosababu ya msingi ya kuishawishi mahakama imwone hana hatia au impunguzie adhabu.
Katika utetezi wake mtuhumiwa alidai kuwa yeye hakutenda kosa hilo isipokuwa ni chuki za mama wa mtoto huyo ambaye alikuwa amemwongezea kodi ya chumba kutoka shilingi 20,000 hadi 40,000 ambazo yeye mshitakiwa alikataa kulipa ongezeko hilo.
Utetezi huo ulipingwa vikali na mwendesha mashitaka wakili wa Serikali ambae aliiomba Mahakama itowe adhabu kali kwa mshitakiwa ili iwe fundisho kwenye jamii kwa watu wenye tabia kama hiyo .
Hakimu Ntengwa baada ya kusikiliza utetezi huo na pingamizi la upande mashitaka alisoma hukumu na kusema kuwa mtuhumiwa amahukumiwa kutumikia jela kifungo cha maisha yake yoye na kama hajaridhika na uamuzi huo anayo nafasi ya kukata rufaa kwenye mahakama ya juu ya ngazi nyingine na kisha alimpatia nakala ya hukumu hiyo na kwenda nayo gerezani.
Mwisho
No comments:
Post a Comment