Na Walter Mguluchuma
Katavi
WAKULIMA wa tumbaku mkoani katavi wamelalamikia kutolipwa fedha za mauzo ya tumbaku huku baadhi ya makampuni yanayonunua tumbaku mkoani humo yameshindwa kununua zao hilo kwamadai kuwa wakulima wamezalisha kuliko uwezo wanunuzi hao.
Wakizungumza na gazeti hili wakulima hao walisema kitendo hicho kimewakatisha tamaa ya kulima zao hilo kwa msimu ujao ambao unapaswa kuanza mwezi Septemba kwa kuotesha mbegu za zao hilo ambalo nitegemeo kwa uchumi kwa wakazi wa Mkoa wa huo.
Akizungumza na gazeti hili mmoja wa Wakulima wa tumbaku wa Chama cha msingi cha ushirika wa wakulima wa tumbaku Mpanda Kati George Ngamila alisema kuwa toka walipo uza tumbaku yao kupitia chama chao cha msingi cha Mpanda kati mwanzoni mwa mwezi Mei mpaka sasa hawajalipwa fedha zao.
Alisema kuwa msimu wa kusia mbegu za tumbaku umeanza tangu mwezi septemba na utamalizika mwezi oktoba lakini wakulima wengi wameshindwa kusia mbegu kutokana na kutolipwa fedha zao za msimu iliopita huku tumbaku nyingine ikiwa imerundikana kwenye maghala ya kuuzia tumbaku na nyingine kwenye nyumba za wakulima hao.
Ngamila alisems kuwa wamekuwa wakipewa taarifa na viongozi wao wa chama cha ushirika cha Mpanda Kati kuwa kuna kilo zaidi ya laki tano hazija nunuliwa na Kampuni ya PREMIUM kutokana na kuzidi kwa uzalishaji wa zao hilo katika msimu uliopita.
Naye Cretus Kagoma mwanachama wa Chama cha msiingi cha Ushirika cha wakulima wa tumbaku cha Katumba alisema kutokana na kutolipwa malipo yao hadi sasa zaidi ya kilo laki nne baadhi ya wakulima wanakabiliwa na ugumu wa maisha.
Aliseama kutoka na kutolipwa fedha zao na wengine kutonunuliwa tumbaku yao na Kampuni ya ununuzi ya TLTC kwa kile kinachodaiwa uzalishaji umezidi malengo waliokubaliana baina ya chama chao cha ushirika na Kampuni ya TLTC wamepoteza kabisa matumaini ya kulima tena Katika msimu ujao.
Alisema kuwa baadhi ya wakulima walikuwa wameingia mkataba na vibarua kuwafanyia shughuli za kilimo hivyo wanaendelea kuwahudumia kwa chakula hadi sasa wakati wakiwa wanasubilia kulipwa malipo yao.
Kwaupande wake meneja wa Chama cha msingi Mpanda Kati Amani Rajabu alieleza kuwa tatizo la tumbaku ya baadhi ya wakulima imesababishwa na wakulima wenyewe kulima zaidi ya makisio yao hali ambayo imesababisha kampuni inayonunua tumbaku kushindwa kununua tumbaku ya ziada.
Akizungumzia suala la malipo ya mauzo yao ya Tumbaku Meneja huyo alisema kuwa wakulima wenyewe waliamua kwenye mkutano wao mkuu kuwa malipo yatakuwa yanafanyika baada ya masoko yote kuwa yamemalizika hivyo kwenye chama hicho bado kuna kilo zaidi ya laki tano ambazo hazija nunuliwa baada ya kuwa zimezidi kwenye makisio yao ya msimu wa kilimo wa mwaka 2016 /2017.
Amani alisema hata hivyo baadhi ya wakulima walisha peleka malalamiko yao kwa Mkuu wa Mkoa huo ambaye aliunda tume ya kuchunguza sababu iliofanya kuwepo kwa ongezeko la ziada la uzalishaji wa zao hilo tofauti na mika iliyopita.
Msimu wa ununuzi wa zao hilo ulianza mwezi mei mwaka huu na ulisimama kuanzia mwezi septemba baada ya kampuni yanayonunua tumbaku kusitisha kununua baada ya kilo walizokuwa wamewekeana mikataba na vyama vya ushirika kuwa zimefikia idadi .
Changamoto ya ongezeko la kilo za tumbaku limetokea katika vyama vyote vya msingi vya ushirika mkoani humo na kusababisha baadhi ya wakulima kushutumiana kuwa tumbaku nyingi iliyouzwa sio ya wakulima bali ni ya walanguzi kutoka mikoa ya jirani na kuiuzia mkoani Katavi .
Mwisho
No comments:
Post a Comment