Wednesday, 13 September 2017

Maombi kwaTundu Lisu yapigwa stop Sumbawanga

Na Gurian Adolf
Sumbawanga
CHAMA cha Demokrasia na maendeleo(CHADEMA) mkoani Rukwa jana kimeshindwa kufanya maombi maalumu kwaajili ya kumuombea mnadhimu na mwanasheria mkuu wa Chama hicho Tundu Lisu ambaye alijeruhiwa kwa lisasi hivi karibuni baada ya jeshi la polisi mkoani humo kuzuia kwa madai kuwa hakiruhusu mkusanyiko.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani humo mwenyekiti wa chama hicho mkoa Sadrick Malila alisema kuwa wameskitishwa sana na hatua ya jeshi hilo kwani suala lakumuombea mwanachama huyo kamwe lisingeweza kusababisha uvunjifu wa amani.

Alisema kuwa Chadema mkoa ilikuwa imewaalika viongozi wa dini kutoka makanisa ya Free Pentecostal Church(FPCT), Kanisa  K. K. T,  Roman Catholic pia na nawachungaji mbalimbali ambao walikuwa tayari wamejiandaa kwaajili yamaombi hayo lakini wamelazimika kusitisha baada ya kamanda wa polisi mkoani humo George Kyando kumwambia mwenyekiti huyo wasitishe maombi hayo. 

Mwenyekiti huyo aliwatangazia wanachama wa Chadema na wananchi wengine wenye walikuwa na nia ya kumuombea Lisu kupitia kusanyiko hilo kuwa kila Mtu afanye maombi binafsi kwani anaamini Mungu ni mwema na atajibu maombi yao. 

Malila alitumia fursa hiyo kuliomba jeshi la polisi kuhakikisha linawasaka watu wanaoitwa kuwa hawafahami waliomjeruhi Lisu kwa lisasi pamoja na afisa wajeshi aliyejuruhiwa kwa kupigwa lisasi juzi jijini Dar es salaam wanasakwa mpaka wapatikane ili kukomesha vitendo hivyo. 

"naliomba sana polisi kama wameshindwa kulinda raia na mali zao,basi waache kulinda mali watalinda wananchi wenyewe wao wawalinde raia tu kwakuwa inawezekana majukumu yamewazidia wabaki na kitu kimoja na wanachi wawasaidie Kitu kingine" alisema.

Naye mwanachama wa chama hicho ambaye pia ni diwani wa viti maalumu wa halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga Martina Lunguya aliwaomba wananchi kutokata tamaa ya kumuombea mwanachama mwenzao ili Mungu amponye upesi aweze kurejea kazini na kuwatumikia wananchi. 

Alisema bila kujali itikadi za kisiasa vitendo vya kupigana lisasi havikubaliki katika nchi yetu kwani si utamaduni na aliwaomba wananchi kuiombea sana nchi kwani vitendo hivyovisipo dhibitiwa vinaweza kusababisha machafuko. 

Hata hivyo kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa alikili kuzuia mkusanyiko huo kwamadai Kuwa mwenyekiti huyo wa chadema aliongea naye lakini hakuomba kibali kwani utaratibu ni kuomba kibali nasi kufanya mkusanyiko bila kibali cha polisi.

Mwisho







No comments:

Post a Comment