Na Gurian Adolf
Sumbawanga
WATU watatu wamekufa katika matukio mawili tofauti likiwemo la wanandugu kumuua ndugu yao kwa kipigo kwamadai ya kuchukizwa kutokana na ndugu yao huyo kutofika kwenye msiba wa marehemu kaka yao aliyefariki baada ya kuugu kwa muda mrefu.
Akitoa taarifa ya matukio hayo kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa George Kyando alisema kuwa tukio la kwanza lilitokea Septemba 12 majira ya saa 07:30 mchana katika kijiji cha Ilemba, kata ya Ilemba,tarafa ya Kipeta, wilayani Sumbawanga.
Alisema wanandugu sita walimvami ndugu yao aitwaye Frank Mwanaharusi(32) nakuanza kumpa kipigo kwamadai Kuwa wamekasilishwa kwanini hakuhudhuria Katika msiba wa kaka yao aliyefariki Septemba 2.
Baada ya kumvamia ndugu yao huyo walianza kumpiga mateke na ngumi sehemu za ubavu wa kulia na kushoto na kumsababishia maumivu makali.
Baada ya kumpiga kwa muda mrefu na kuona kuwa amezidiwa waliamua kumuacha na kukimbia kusiko julikana na kumuacha ndugu yao katika maumivu makali mpaka akafariki dunia.
Kamanda Kyando alisema siku hiyo hiyo majira ya saa 12:30 jioni Katika kijiji cha Chala katika barabara ya Namanyere Sumbawanga wilaya ya Nkasi gari lenye namba za usajili T 232 BDG HOWO MIXER likiwa limebeba zege lilipinduka na kusababisha vifo vya watu wawili waliofahamika kwa majina ya Shabani Supa(31) mwenyeji wa mkoa wa Tabora na Gudence Ernest(33) mwenyeji wa mkoa wa Singida.
Chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa gari hilo ambapo dereva alishindwa kulimudu gari hilo lilipinduka nakusababisha vifo hivyo.
Watuhumiwa wa matukio hayo walikimbia na wanasakwa na polisi iliwachukuliwe hatuaza kisheria.
Mwisho
No comments:
Post a Comment