Thursday, 14 September 2017

Waaswa kuiombea nchi amani

Na Gurian Adolf
Sumbawanga
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Zelote Stephen amewaomba  waumini wa madhehebu yote yaliyopo mkoani humo kuendelea kuiombea nchi amani kwani serikali ipo imara katika kuhakikisha inasimamia misingi ya sheria. 

Ombi hilo alilitoa jana wakati alipokuwa akifungua mkutano wa siku nne wa Sinodi ya kanisa la Moravian jimbo la Rukwa na Katavi, mkutano ambao umehudhuriwa na wachungaji, makatibu, wenyeviti na wanakwaya wa mikoa yote miwili.

Alisema watanzania ni watu wanaomuamini mwenyezi mungu hivyo basi kila mtu ahakikishe anaiombea sana nchi yetu na viongozi wake ili amani iliyopo iendelee kudumu. 

"Kama viongozi wa dini mna silaha kubwa ya kuiombea nchi amani hivyo tunawaomba muendelee kuombea nchi amani na kuwasisitiza waumini wafanye hivyo na niwahakikishie kuwa serikali ipo imara kuhakikisha sheria zinafuatwa ili kuendeleza amani iliyopo."

kwa upande wake mgeni mwalikwa Askofu wa kanisa Katoliki Jimbo la Sumbawanga  Damian Kyaluzi aliipongeza serikali kwa kuthibiti yaliyotokea katika wilaya ya kibiti, na kukemea yaliyowatokea Mh. Tundu Lisu pamoja na Meja Generali Mstaafu Mrimbata na kuendelea kuwaombea na kuliombea taifa liendelee kubaki na amani iliyoachwa na waasisi wa nchi hii.

awali akisoma risala fupi ya kanisa hilo kwa mgeni rasmi mwenyekiti wa kanisa la Moravian jimbo la Rukwa mchungaji Nobrt Sikazwe alilalamikia ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga kushindwa kuwapa vibali vya ardhi ili waendelee kushirikiana na serikali katika kuleta maendeleo.

Mwisho

No comments:

Post a Comment