Na Israel Mwaisaka
Nkasi
KIJANA aliyetambulika kwa jina la Venance Kuchangwa(24) mkazi wa kijiji cha Miyombo kata ya Mashete wilayani Nkasi mkoani Rukwa amejinyonga hadi kufa kwa kutumia kamba ya nguo yake kwamadai kuwa hela hazi patikani.
Akithibitisha tukio hilo afisa mtendaji wa kata ya Mashete, Cresence Sinkamba alisema kuwa kijana huyo alikutwa amekufa jana majira ya saa 9 alasiri akiwa amejitundika juu ya mti.
Alisema awali kijana huyo aliamua kuacha shule ya sekondari kidato cha tatu na kwenda kufanya kazi za kubeba mizigo ambazo aliamini kuwa zinaweza kubadilisha maisha yake.
Alisema Kuwa baada ya kufanya kazi hizo kwa muda mrefu hakupata mafanikio yoyote zaidi alikuwa akilalamikia ugumu wa maisha na baadaye aliamua kuoa mke huku wazazi wake nao wakiwa wanamtegemea yeye hivyo kujikuta akiwa na mzigo mkubwa wakumtunza mke wake na wazazi pia.
Hivyo kifo hicho kimehusishwa na ugumu wa maisha kutokana na malalamiko ya mara kwa mara aliyokuwa nayo hasa baada ya kuamua kuoa kwani alikuwa akilalamika hela hazipatikani Siku hizi tofauti na miaka iliyopita.
Sinkamba alisema kuwa kilichopelekea ugumu zaidi wa maisha kwa kijana huyo ni kwa kutegemea kazi moja tu ya kubeba mizigo na kuacha kujishughulisha na kilimo kitu ambacho ingekuwa ni ngumu kwake kupata unafuu wamaisha licha ya wao kumshauri kujishirikisha na suala la kilimo lakini alikuwa akikataa.
Baada ya polisi kuufanyia uchunguzi mwili huo wa marehemu walikabidhiwa ndugu zake kwaajili ya mazishi ambapo jana yalifanyika mazishi yake kijijini hapo.
Mwisho
No comments:
Post a Comment