Wednesday, 2 August 2017

Wanaswa na vito vya thamani

Na Gurian Adolf
Sumbawanga
Jeshi la polisi Mkoani Rukwa limekamata maboksi mawili yenye vito vinavyosadikiwa kuwa ni vya thamani pamoja na mchanga mweusi kutoka kwa raia wa nchi ya jirani ya Kongo ambavyo vilikuwa vikiingizwa nchini kimatendo  kwa kisingizio cha kuvileta katika maonesho.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando alisema kuwa tukio la kukamata vito hivyo lilitokea Julai 29 majira ya saa 4 za asubuhi wakati askari polisi  wakiwa na askari wa Uhamiaji wakiwa katika doria. 
Alisema kuwa askari hao kwa pamoja walifanikiwa kukamata raia wawili wa Congo wakiwa na maboksi hayo yenye vipande vya mawe na mchanga mweuzi wenye uzito wa gramu 500 ambapo raia hao wa Congo wamesema kuwa mawe hayo yanayaingiza nchini kwa lengo la kufanya sanaa za maonesho. 
Kamanda Kyando alisema kuwa ni makosa kuingiza nchini madini na vitu vya thamani bila kufuata taratibu za nchi kwani kunasheria ambazo zinatoa mwongozo katika suala hilo. 
Alisema kuwa watuhumiwa hao wanashikiliwa na polisi na watafikishwa mahakamani wakati wowote pindi upelelezi utakapo kamilika. 
Mwisho

No comments:

Post a Comment