Sumbawanga
WAANDISHI wa habari mkoani Rukwa wameshauliwa kujituma Katika kufahamu mambo mengi zaidi ili waweze kuwasaidia wananchi wanapokabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya mawasiliano ili waweze kuendana na kasi ya kimabadiriko ya kiteknolojia.
Ushauri huo umetolewa jana na naibu wa mkurugenzi wa idara ya watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano mamlaka ya mawasiliano Tanzania Thadayo Ringo wakati akitoa mafunzo ya namna ya kuhama mtandao wa simu bila kubadirisha namba ya simu kwa waandishi wa habari wa mkoa huo.
Alisema kuwa miongoni mwa makundi ambayo yanapaswa kusoma sana na kufahamu mambo mengi ni waandishi wa habari kwani jamii inategemea kupata ufafanuzi wa vitu vingi na kwausahihi kutoka kwao.
Ringo alisema kuwa kila mwana habari ajitahidi kusoma sana na kujifunza vitu tofauti kwakua asipofahamu kunauwezekano mkubwa wa kuipotosha Jamii kwani wanauwezo mkubwa wa kuifikia na inawanawasikiliza wao kila siku.
Naye Mhandisi wa mamlaka hiyo FĂ©licien Mwesigwe alisema kuwa wananchi wanawajibu mkubwa wa kutumia teknolojia za kisasa kwani zinawasaidia Katika kurahisisha mambo na kufanya vitu vingi kwa wakati mmoja.
Alisema kuwa pamoja na kuwa teknolojia inachangamoto mbalimbali lakini mamlaka hiyo inajitahidi kuzikabili changamoto hizo pindi zinapojitokeza ili kuondoa usumbufu kwa wananchi.
Mwisho
No comments:
Post a Comment