Nkasi
SERIKALI wilayani Nkasi mkoani Rukwa imewaonya walimu wa shule za msingi na sekondari wilayani humo kuacha tabia ya kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi wao.
Mkuu wa wilaya hiyo Said Mtanda alitoa onyo hilo kwa walimu hao jana wakati akizungumza katika kikao cha kazi huku akiwatuhumu baadhi ya walimu kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi wao.
Alisema kuwa miongoni mwa mambo ambayo yanamuudhi yeye akiwa ni mkuu wa wilaya hiyo ni tabia ya walimu kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi kwani tabia hizo zinawahairibia wanafunzi hao ndoto zao za baadae.
"Ole wake mwalimu yeyote atakayebainika kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanafunzi,serikali ya wilaya itahakikisha mwalimu huyo anachukuliwa hatua kari kwani hatupo tayari kuwaendekeza walimu wa aina hii katika wilaya ya Nkasi"..alisema
Aliwaonya pia wanaume wote wilayani humo kuacha tabia ya kuwalaghai wanafunzi na kuwa na mahusiano nao ya kimapenzi kwani ni tabia mbaya na yeye ataongoza vita ya kupambana na wanaume wote wenye tabia hiyo.
Aidha Mtanda aliwataka walimu wilayani humo kuongeza bidii katika suala la kufundisha kwani anataka wilaya hiyo ifanye vizuri kitaifa kwakuwa inawalimu waliosoma katika vyuo ambavyo walimu wa mikoa mingine inayoongoza wamesoma sasa kwanini wilaya ya Nkasi isiongoze kitaifa.
Naye mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Nkasi Julius Kaondo aliwataka watendaji wilayani humo kujituma katika kufanya kazi hususani katika suala zima la kukusanya mapato ambayo yanaiwezesha serikali kuwahudumia wananchi.
Alisema kuwa kila mtendaji ahakikishe kuwa mapato ya serikali yanaifikia serikali kwani sasa hivi serikali ya awamu ya tano imeamua kuwatumikia wananchi kwa dhati hivyo wasiwepo wajanja wachache ambao wataiangusha serikali kwani kila mwananchi anahaki ya kufaidi ukwasi wa halmashauri ya Nkasi na taifa kwa ujumla.
Alisema kuwa serikali hivi sasa inaboresha ujenzi wa barabara, afya,maji elimu na maeneo mengine itaweza kufikia malengo yake iwapo wananchi watalipa mapato na watendaji watayakusanya na kuhakikisha yanaifikia serikali na hatimaye kuwanufaisha wananchi wote.
Mwisho
No comments:
Post a Comment