Na walter Mguluchuma
Mlele
SERIKALI imeipandisha hadhi zahanati ya Inyonga iliyopo wilaya ya Mlele mkoani Katavi nakuwa hospitali ya wilaya baada ya kukidhi vigezo ili iwezekutoa huduma kwawananchi wa wilaya hiyo.
Waziri wa afya,Maendeleo ya Jamii,jinsia wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameipandisha hadhi Zahanati hiyo jana mara baada ya kuikagua na kuridhishwa na vigezo vinavyo takiwa vya kuipandisha hadhi Zahanati hiyo kuwa hospitali ya Wilaya.
Alisema amefikia maamuzi y'a kuipandisha hadhi zahanati hiyo kuwa Hospitali ya wilaya kutokana na mamlaka aliyonayo kama Waziri wa Wizara husika.
Alivitaja baadhi ya vigezo vinavyofanya iwe na hadhi ya hospitali ya Wilaya kuwa ni huduma ya upasuaji ,Chumba cha kuhifadhi maiti , maabara , huduma ya maji,umeme wa uhakika na huduma ya damu.
Alifafanua kuwa kama zahanati hiyo inatowa huduma kama hospitali ya wilaya kwanini yeye kama Waziri mwenye dhamana ashindwe kuipandisha hadhi Zahanati hiyo na ukiangalia pia Wilaya hiyo haina Hospitali.
Mwalimu alisema rais John Magufuli alisha waagiza Mawaziri kuwa na uamuzi wa kutoa maamuzi magumu pale panavyositahili kama ambavyo alivyofanya yeye kuipandisha hadhi Zahanati hiyo.
Alitoa ahadi ya kupeleka wataalamu wengine haraka wezekanavyo wenye hadhi ya kufanya kazi kwenye Hospitali hiyo haraka iwezekanavyo kabla ya mwezi wa Septemba hauja kwisha .
Waziri huyo alikabidhi kwa niaba ya rais magodoro 20,vitanda 20 shuka 50 na vitanda vitano vya kisasa vya kujifungulia akina mama wajawazito kwa kwaajiri ya Hospitali hiyo ya Wilaya.
Nae Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Dkt Luccy Kafumu alieleza kuwa mchakato wa maombi wa kuipandisha hadhi zahanati hiyo ulianza toka mwaka 2013 baada ya wao kuona inasitahili kuwa Hospitali ya Wilaya .
Dkt Kafumu alieleza kuwa Zahanati hiyo kwa muda wote toka mwaka 2013 imekuwa itoa huduma kama hospitali ya Wilaya kwa kitendo hicho cha kuipandisha hadhi kitasaidia hata Mapato ya kununua dawa kuongezeka kwenye bajeti ijayo.
Mwisho
No comments:
Post a Comment