Sunday, 16 July 2017

Shirika la Reli nchini laagiza kuongeza mabehewa ya mizigo Mpanda

Na  Walter Mguluchuma
Katavi
 Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika  la  reli  nchini TRL  wameliagiza  Shirika  la  reli nchini  kuhakikisha  inapeleka  mabehewa  ya  mazigo ya  kutosha  katika  Stesheni ya  Mpanda  kwa  ajiri ya kusarisha  mazao ya  mahindi na mpunga yaliyokwama  kusafirishwa  kutoka  mjini Mpanda mkoani Katavi na  kupelekwa  kwenye  maeneo  yenye upungufu wa  chakula hapa nchini.
Agizo  hilo  lilitolewa jana  na  Wajumbe   wa  bodi  hiyo   walipoitembelea  stesheni  ya  Mpanda  na kushitushwa  na  mrundikano  wa  mazao ya   mahindi  na mpunga  yaliokwama  kusafirishwa kutokana  na  upungufu  wa mabehewa  ya  mazigo.
Mwenyekiti  wa  bodi   ya  TRL   Prof  John  Kondoro  alisema   yapo  baadhi ya  maeneo    hapa  nchini   yana  upungufu mkubwa wa  chakula  hivyo  ni   lazima  mazao   yalio   rundikana   katika  stesheni ya  Mpanda  kwaajiri ya upungufu  wa  mabehewa  ya  mizigo yakasafirishwa  haraka  na  kufika  kwenye  maeneo yanako  safirishwa.
Alifafanua  kuwa  wao  wajumbe  wa bodi   hawakuwa   wanajua  kama  kuna   mrundikano mkubwa  wa  kiasi  hicho   cha  mazao  ya   mahindi  na mpunga   hivyo ziara  yao  ya  siku  moja  imewasaidia  kutambua  tatizo  ambalo  lipo  ndani ya  uwezo wa  TRL.
Mkurugenzi  Mkuu  wa   TRL   Masanja   Kadogosa   aliwahakikishia   wajumbe   wa    bodi  hiyo  kuwa   tatizo  hilo  atalishughulikia   na  ndani  ya  kipindi  cha   wiki  moja kuanzia  sasa   hakutakuwa  na   mlundikano  wa  mazao  kwenye  stesheni  hiyo ya  Mpanda  na kuwaahidi mazao  yote yatakuwa  yamesafirishwa.
Alimwagiza  mkuu wa  kitengo  cha  TRL   anae  husika kusafirisha  mizigo  waliyekuwa  nae  kwenye   ziara   hiyo  abaki   mijini Mpanda mpaka  hapo mazao yaliorundikana  kwenye   stesheni  yatakapokuwa  yamesafirishwa  yote.
Pia  Mkurugenzi   Mkuu  huyo wa TRL alisema kuwa shirika hilo linatarajia  kuongeza  safari  za   treni ya  abiria  kutoka   tatu  kwa  wiki  hadi kuwa  nne  kutoka mkoani   Tabora kwenda mjini   Mpanda   mkoani Katavi kutokana na  kuongezeka  kwa   idadi  ya  abiria wakati  huu wa  kipindi  cha  kiangazi.
Aidha  alisema kuwa wanaangalia  uwezekano  wa  kuleta  behewa  la   daraja  la  kwanza  la  abiria na  endapo kama   itaonekana  kuna   mahitaji  ya  abiria  wa  kutosha wanao  hitaji  kufafiri kwa    daraja  hilo la  kwanza.
Mwisho

No comments:

Post a Comment