Sumbawanga
LICHA ya halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa kutangaza kutolipa fidia kwa wakazi wa Chanji ambao watapisha ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami utakaojengwa kati ya Majengo hadi Chanji katika mji wa Sumbawanga, mbunge wa jimbo la Sumbawanga mjini Aesh Hilary ameagiza kuwa ni lazima watu hao walipwe fidia na yeye yupo tayari kusimamia kwani hayupo tayari kuona mwananchi anavunjiwa nyumba yake bila kulipwa fidia.
Mbunge wa jimbo la Sumbawanga Aesh Hilary akiwahutubia wakazi wa Chanji mjini Sumbawanga
Agizo hilo alilitoa jana katika eneo la Soweto Chanji wakati akihutubia mamia ya watu waliojitokeza kumsikiliza alipokuwa akizungumza na wananchi wa Chanji ambapo pia alitumia fursa hiyo kujibu kero mbalimbali za wananchi wa eneo hilo.
Moja kati ya kero zilizo wasilishwa kwa mbunge huyo ni malalamiko ya baadhi ya wananchi ambao watavunjiwa nyumba zao kwa madai kuwa wanapaswa wapishe ujenzi wa barabara itakayo jengwa kwa kiwango cha lami kutokea Majengo mpaka kuunganisha na barabara iendayo mkoani Mbeya.
Alisema kuwa sio haki kumvunjia mwananchi nyumba yake hata kama itakuwa ni sehemu ya nyumba ni lazima alipwe fidia na yeye mwenyewe atasimamia kwani hayupo tayari kuona mtu anavunjiwa nyumba bila kulipwa fidia yoyote.
Wakazi wa Chanji Soweto mjini Sumbawanga wakimsikiliza mbunge wao Aeshi Hilary
Mbunge huyo alisema kuwa kitakua sio kitendo cha uungwana kuvunja nyumba ya mwananchi bila kulipa fidia, alisema kuwa ni lazima halmashauri ya Manispaa itafute fedha za kulipa fidia naye atahakikisha wananchi hao wanapatiwa haki yao.
Alisema kuwa maendeleo ni kitu kizuri lakini pia lazima haki itendeke na si kuwatia hasara watu wengine kwa sababu ya ujenzi wa barabara kwani walitumia fedha zao wakati wa ujenzi wa nyumba hizo na si busara kuvunja halafu wasilipwe fidia.
"Ndugu zangu ninani ambaye wangekuwa tayari kuvunjiwa hata sehemu ya nyumba yake bila kulipwa fidia kwa madai kuwa tunajenga barabara?, naamini hakuna sasa iweje wananchi hawa wa Chanji wao wasilipwe fidia...nitahakikisha wanapata haki yao kwani Mimi mbunge wao sipo tayari kuona hilo"... Alisema Hilary.
Kuhusu suala la kulima karibu na vyanzo vya maji alisema kuwa katika hilo hayupo tayari kuunga mkono ni lazima sheria ifuatwe wanaolima bustani wanapaswa kuacha umbali wa mita 6o kwani ndivyo sheria inavyo elekeza na nilazima iwe hivyo vinginevyo vyanzo vya maji vitakauka na wananchi watapata shida ya maji.
Aidha aliwasihi wananchi wa eneo hilo kuheshimu sheria za nchi na iwapo kuna jambo ambalo hawaridhiki nalo waende ofisini kwake kwani yupo yeye mbunge wao ambaye yupo kwaajili ya kuwasaidia katika changamoto mbalimbali na iwapo hawata mkuta yeye yupo katibu wake na atawasikiliza na kuwasiliana na mbunge wao kisha ufumbuzi wa tatizo lao utapatikana.
Mwisho
No comments:
Post a Comment