Thursday, 20 July 2017

Laki tano zamuokoa kwenda jela

Na Gurian Adolf
Katavi
ALIYEKUWA askari wa Jeshi la Polisi mwenye cheo cha Konsitebo  Peter Kashuta wa Kituo cha Polisi Mwese  wilayani Tanganyika katika mkoa wa Katavi  amenusurika kwenda jela miaka mitatu baada ya kulipa faini mahakamani kiasi cha Shilingi laki 5.
Fedha hizo alizitoa baada ya Mahakama ya Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi baada ya kumtia hatiani na
kumuhukumu  kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela au  kulipa faini hiyo kwa kosa la  kuomba na
kupokea rushwa  kiasi cha Shilingi laki 7
Akisoma hukumu hiyo hakimu Mkazi mfawidhi wa  Mahakama  ya  wilaya ya Mpanda Chiganga Ntengwa
alieleza kuwa ameridhika na ushahidi uliotolewa upande wa mashataka
ambao haukuacha shaka  yoyote kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo.
Alisema kuwa makosa ya kuomba na kupokea rushwa yanakwenda sambamba
isipokuwa Mahakam hiyo imemtia hatiani  kwa kosa la kupokea
rushwa ambapo  upande wa mashtaka uliita mashahidi wanne.
Akitoa hukumu hiyo Hakimu Ntengwa alisema kuwa mshtakiwa ametiwa
hatiani kwa mujibu wa kifunngu cha Sheria namba 15 cha Sheria ya
kupambana na kuzuia rushwa  sura ya 11 ya 2007.
Awali waendesha mashtaka wa Takukuru Bahati Haule akisaidiwa na
Simon Buchwa walidai mahakamani hapo  kuwa mshtakiwa alitenda kosa
hilo Februari 09 mwaka jana katika kijiji cha Mwese kilichopo katika
wilaya ya Tanganyika katika mkoa wa Katavi .
Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa siku hiyo ya mshtakiwa aliomba
rushwa kiasi cha shilingi laki 7 kutoka kwa Luchega Mambalu ambaye
alikuwa amefunguliwa  jarada la kesi  katika Kituo cha Polisi Mwese.
 Katika  utetezi  wake   Mahakamani  hapo  mshitakiwa     alidai kuwa  yeye  hakutenda  kosa  hilo  kwani  siku  hiyo   maafisa wa  Takukuru   hawakumkamata  na  fedha  yoyote  ile.
 Madai hayo yalipingwa   vikali na  waendesha  mashitaka  wa  Takukuru kwa  kile   walichodai kuwa  kitendo cha  mshitakiwa  kukimbia  na  alipokamatwa hakukubali  na   badala  yake   alianza  kuwapiga makonde  maafisa  hao wa Takukuru na  kisha  alifanikiwa kuzitupa fedha  hizo   ambazo  zilikuwa ni kielelezo  kwenye  kesi  hiyo ambazo zilikua  ni  ushahidi tosha  wakumtia  hatiani.
Hata  hivyo   aliweza  kulipa   faini ya  Tshs  500,000 na  kusalimika  kutumikia  kifungo cha  miaka   mitatu  jela.
Mwisho

No comments:

Post a Comment