Na Gurian Adolf
Sumbawanga
TABIA ya baadhi ya wakazi mkoani Rukwa ya kuendelea kujichukulia hatua mkononi bado inaendelea kuota mizizi mkoani humo ambapo watu watatu wameuawa na kisha miili yao kuchomwa moto wakituhumiwa kwa wizi wa ng'ombe 16.
Tukio hilo lilitokea katika kijiji cha Mao kata ya Mbuluma wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa ambapo watuhumiwa hao walidaiwa kuwa wameiba ng’ombe 16 wa Mtokambali Nsosomo.
Akizungumza na gazeti hili diwani wa kata hiyo Saidi Manoti, alisema kuwa wezi hao walikuwa wametokea katika kijiji Nchenje wilaya jilani ya Nkasi na kwenda kuiba ng'ombe hao katika kijiji jirani cha Mao.
Alisema baada ya kufanikiwa kuiba ng'ombe hao na kuanza kuondoka nao kutoka katika kijiji hicho majira ya usiku wa manane ndipo wakazi wa kijiji hicho walipo amshana na kwenda kuwakamata wezi hao.
Baada ya kuwanyemelea walifanikiwa kuwazingira ndipo walipowakamata na kisha kuwapa kipigo hali iliyowafanya washindwa kukimbia ndipo walipo wachoma moto wezi hao na kuwaua kabisa.
Aidha alisema kuwa watu hao hawakutambulika majina wala makazi yao licha ya kuwa walidhaniwa kuwa wametikea katika vijiji vya jirani na walipokwenda kufanya wizi huo wa mifugo.
Diwani huyo alisema kuwa na kuwa kutikana na kuendelea kushamiri kwa mauaji hayo holela anaandaa utaratibu wa kuitisha mikutano ya hadhara katika kata yake ili kutoa elimu kwa wananchi juu ya kuachana na vitendo vya kujichukulia sheria mkononi kwa kisingizio kuwa ni wananchi wenye hasira Kali.
Kwa upande wake Kamanda wa polisi mkoani Rukwa Geoge kyando, amekiri kutokea kwa mauaji hayo ya watu sita na kuongeza kuea tayari baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mao wamekamatwa na watafikishwa mahakamani pindi upelelezi utakapo kamilika.
Aidha ameendelea kuonya tabia hiyo ya kujichukulia sheria mikononi kwa kuwaua watuhumiwa kwa kisingizio kuwa ni wananchi wenye hasira Kali.
Mwisho
No comments:
Post a Comment