Na Walter Mguluchuma
Katavi
WANANCHI wa madhehebu mbalimbali waliopewa uraia wa Tanzanzia ambao awali walikuwa ni wakimbizi kutoka nchi y'all Burundi na walikuwa wakiishi katika makazi ya Wakimbizi ya Katumba Wilayani Mpanda Mkoani Katavi jana wamefanya Ibada maalumu kwa lengo la kumuombea Rais John Magufuli ili Mungu azidi kumpa ujasili wa kupambana na watu wanaohujumu rasrimali za nchi ya Tanzania.
Ibada hiyo ilifanyika katika eneo la Kijiji cha Myaki katika Makazi ya Wambizi ya Katumba ambapo walimualika pia Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Richald Mbogo.
Paroko wa Kanisa Katoliki Parokia ya Katumba Padri Benedict Baritoya alisema kuwa kazi ya kupambana na watu wanaohujumu rasilimali za nchi inayofanywa na Rais Magufuli sio ndogo ndiyo maana wameamua kumfanyia maombi maalumu ya kumwombea ili Mungu azidi kumpatia ujasiri asikate tamaa.
Alisema Watanzania wanakilasababu ya kuiombea Serikali inayoongozwa na rais Magufuli kutokana na kazi kubwa anayofainya ya kusimamia raslimali kwani imeweza kuwafumbua macho Watanzania waliokuwa hawaoni na waliokuwa hawasikii wamesikia.
Padri Baritoya alieleza mbali ya viongozi kuwa na watu wa kuwalinda lakini ulinzi wa Mungu bado ni muhimu ili kusiwe na mtu wa kuzuia jitihada zake hivyo wasipo waombea viongozi taifa linaweza kufarakana.
Naye Mchungaji wa FPCT Alfed Mbaruku alisema kama viongozi hawasimamii haki maendeleo hayata kuwepo na Mungu anataka haki itendeke Tanzania kama ambavyo anavyofanya Magufuli kwa kuwajari maskini pasipo kuwabagua.
Hivyo Wanzania wanakila sababu ya kuiombea nchi amani na kumbombea Rais na viongozi wote anao waongoza wafanya kazi kwa manufaa ya Wanzania wote .
Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Richald Mbogo alisema jambo la kumwombea Rais na viongozi wanaomsaidia kuongoza Serikali liwelinafanyika mara kwa mara kwenye Makanisa, Miskitina kila Mtanzania nyumbani kwake kwani magezi anayoyafanya sio kila mtu anayafurahia.
Alisema rais toka ameingia madarakani amekuwa mstari wa mbele katika mageuzi ya kuongeza mapato ya nchi, kusimamia raslimali za nchi kuwabana mafisadi na kusimamia sheria za madini zimeweza kubadilishwa hivyo vita ya kutaka kuharibu jitihada hizo sio za ndani ya nchi tuu bali hata nje ya nchi pia.
Mwisho
No comments:
Post a Comment