Saturday, 22 July 2017

Zelote Steven asikitishwa na watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga

Na Gurian Adolf
Sumbawanga
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Zelote Steven amesikitishwa na kitendo cha halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa kuwa na hoja za kujibu zipatazo 60 ambazo zimesababisha halmashauri hiyo kupata hati ya mashaka wakati halmashauri hiyo imeajiri watumishi wenye  uwezo ni hujuma  dhidi ya watendaji hao.
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Zelote Steven akilihutubia baraza la  madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga

Akizungumza katika kikao cha baraza la dharula la  madiwani Jana Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa anasikitishwa sana na kitendo hicho kwani wataalamu hao wameajiriwa huku serikali ikiwa  inamatumaini kuwa ni watu wenyeuwezo sasa zinapotokea hoja hizo yeye binafsi zinamsikitisha sana.
Alisema kuwa halmashauri hiyo haipaswi kuwa na huruma na watu wote waliosababisha hoja hizo kwani wanaoumia  ni wananchi kutokana na baadhi ya watendaji kusababisha hali hiyo ambayo inapelekea halmashauri kupata hati ya mashaka na hata chafu na yeye akiwa ni Mkuu wa mkoa hatakubaliana na hilo.
"Binafsi nachukizwa sana na hali hii, siipendi  hata kidogo kwani inaumiza na kuonekana hatuna watendaji wenyeuwezo, abadani sitakubali hali hii katika mkoa wangu labda uwe mkoa mwingine"... Alisema.
Alisema kuwa madiwani wanapaswa  Ku tambua kuwa wao ndio taa ya halmashauri hiyo kwani wakilegalega na halmashauri ikiendelea kupata hati ya mashaka wajue watakwenda kujibu wenyewe kwa wananchi ambao wamewatuma kuwawakirisha.
Kwa upande wake mwenyekiti wa baraza hilo la  madiwani Kalolo Ntila alisema kuwa hoja hizo hazikutokana na baraza lililopo hivi sasa la  madiwani na hata mkurugenzi aliyopo  hivi sasa na aliahidi kuwa wale wote waliosabaisha hoja hizo lazima watafutwe popote  waliopo na wachukuliwe hatua.
" hatutawaacha watu hawa bali tunazipitia hoja moja baada ya nyingine na kuzitolea majibu,lakini zile ambazo kitakuwa na matatizo ni lazima waliopo sababu sha wasakwe popote  walipo  na hatua dhidi yao zichukuliwe" alisema 
Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Rukwa.

Awali akizungumza katika baraza hilo la  madiwani mkaguzi mkazi na mdhibiti wa hesabu za serikali John Nalwambwa alisema kuwa ofisi yake ilibaini kuwepo kwa hoja 60 zenye utata ambapo hoja 25 kati ya hizo ndizo  zilizopelekea kupata hati ya mashaka.
Alisema kuwa kuna fedha zaidi ya shilingi milioni 40 ambazo hazieleweki vizuri matumizi yake na baadhi ya vitabu vya makusavyo vikiwa  vimepotea na hivyo nilazima  ifahamike hatma ya suala hilo.
Alisema kuwa ofisi yake imefanya  kazi kwa weledi mkubwa bila kuonea  mtu  na ndiyo imebaini hayo hivyo basi ni jukumu la halmashauri kuona ni jinsi gani itajibu hoja hizo ili zisijirudie tena.
Mwisho

No comments:

Post a Comment