Saturday, 22 July 2017

Baraza la madiwani Sumbawanga lakutana kujadili hati ya Mashaka

Na Gurian Adolf
Sumbawanga
BARAZA la  madiwani la  Halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa leo limekaa  kikao cha dharula baada ya kupata hati ya mashaka kutoka kwa mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali(CAG)
Akifungua kikao hicho cha dharula mwenyekiti wa halmashauri hiyo Kalolo Ntila  alisema kuwa pia wamewaalika wajumbe kutoka katika serikali ya mkoa wa Rukwa wakiongozwa na Mkuu wa mkoa huo Zelote Steven kwaajili ya kuhudhuria kikao hicho maalumu.
Mwenyekiti wa baraza la halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga Kalolo Ntila  akifungua baraza la  madiwani

Alisema kuwa lengo la  kuitisha baraza hilo ni kujadiri hoja likizo wasilishwa na mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali ambazo zimepelekea halmashauri hiyo kupata hati ya mashaka ambapo shilingi zaidi ya shilingi milioni 40 zilikuwa hazina  maelezo ya kutosheleza pamoja na upotevu wa vitabu vya makusanyo.

Mkaguzi na mdhibiti wa ndani aliwasilisha hoja 60 ambapo kati ya hoja hizo ni hoja 25 ndizo zilizopelekea halmashauri hiyo kupata hati hiyo ya mashaka.

Alisema kuwa pamoja na mambo hayo yapo mambo mengine ambayo yanapaswa  yatolewe majibu kwani ndiyo yaliyopelekea mkaguzi mkazi awape hati hiyo ya mashaka katika ukaguzi wa hesabu za mwaka 2016 na ni vizuri zikapatiwa majibu.

Ntila  alisema kuwa ni jukumu la madiwani hao kuangalia kwa makini mwenendo wa halmashauri hiyo ili hati ya namna  hiyo isije  kutokea tena kwani hawafurakii kupata hati chafu wala ya mashaka wao wanashauku ya kupata hati safi.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga John Msemakweli akizungumza katika baraza la  madiwani

"Ndugu zangu madiwani wenzangu  naamini kuwa hakuna anayependa kupata hati chafu wala ya mashaka bali  ni faraja ya kila mtu diwani na watendaji kuona kuwa tunapata hati safi"... Alisema Ntila.
Alisema kuwa wao kama madiwani wametumwa na wananchi hivyo basi wanapaswa kuhakikisha halmashauri yao inakwenda  vizuri ili hati ya mashaka isije  kujirudia tena.
Mwenyekiti huyo wa halmashauri huyo alisema kuwa wanaimani kubwa na watendaji wa halmashauri lakini pia wanapaswa kuhakikisha wa najua kila kitu kwani kujua kwao ndio wananchi wamejua  kwakua wanawawakilisha wao.
Baadhi ya madiwani wa baraza la  halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga wakiwa kwenye kikao chao

Baadhi ya wataalamu wa halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga,pamoja na wageni waalikwa wakifuatilia kwa makini kikao cha baraza la  madiwani

Awali akimkaribisha mwenyekiti huyo kufungua kikao hicho cha baraza la  madiwani mkurugenzi wa Halmashauri hiyo alisema washukuru  madiwani hao kwa kuhudhuria kikao hicho kwa wingi ili kuweza  kufahamu  hoja hizo na anaamini  zitapatiwa majibu na hati hiyo yenye mashaka haitatokea tena.
Mwisho

No comments:

Post a Comment