Na Walter Mguluchuma
Katavi
Mtu mmoja amekufa hapo hapo na wengine 13 kujeruhiwa na kulazwa katika hospitalini ya wilaya ya Mpanda mkoani Katavu baada ya basi walilokuwa wakisafirilia kuacha njia na kupinduka kutokana na mwendo kasi ambao dreva alikua akiendesha.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Damas Nyanda alisema ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa 5:30 katika Kijiji cha Ikondamoyo Tarafa ya Nsimbo Wilaya ya Mpanda barabara ya Tabora kwenda Mpanda Mkoani Katavi.
Alimtaja marehemu aliyefariki kuwa ni Paulo Mussa (37) Mkazi wa Wilaya ya Meatu Mkoani Shinyanga alifariki hapo hapo baada ya ajari hiyo kutokea.
Kamanda Nyanda alisema kuwa ajari hiyo ililihusisha basi la Kampuni ya ALLYS,S lenye Namba za usajiri T473 CCC aina ya Scania lililokuwa likiendeshwa na Dreva anaeitwa Jushua Bebedictor(45)mbaye alikimbia baada ya ajali hiyo.
Alieleza mara baada ya ajari hiyo majeruhi wote 13 walichukuliwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Manispaa ya Mpanda ambako wanaendelea kupatiwa matibabu huku majeruhi wanne hari zao zikiwa si nzuri.
Kamanda NYanda alisema kuwa chanzo cha ajari hiyo kilisababishwa na mwendo kasi wa dreva ambae gari lilimshinda kukata kukona kutokana na kuwa kwenye mwendo kasi na kuacha njia na kisha kupinduka.
Baada ya dreva kukimbia jeshi la polisi lilifanya msako wa kumsaka na waliweza kufanikiwa kumkamata na mpaka sasa wanaendelea kumshikilia kwa mahojiano zaidi na mara uchunguzi utakapo kuwa umekamilika atafikishwa mahakamani ili akujibu mashitaka yanayomkabili.
Kamanda Nyanda ametowa wito kwa madereva kuacha tabia ya kuendesha magari kwa mwendo kasi na kuwataka wazingatie sheria za usalama barabarani.
Mwisho
No comments:
Post a Comment