Na Gurian Adolf
Sumbawanga
WAKAZI wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa wameshauriwa kulipa kodi kwa wakati na bila mizengwe ilikuiwezesha serikali kupata mapato ambayo itayatumia katika bajeti hali ambayo itaisaidia nchi kuacha kutegemea misaada kwa kiasi kikubwa kutoka kwa wahisani.
Dkt Joseph Chintowa akimkabidhi funguo ya gari mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga Kaloro Ntila.
Hayo yameelezwa Jana na Dkt Joseph Chintowa,mkurugenzi wa ufundi wa shirika lisilo la kiserikali la walter reed wakati akikabidhi gari aina ya Toyota Lendruiser lenye thamani ya shilingi milioni 150, kwa halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga ambalo litatumika katika miradi inayohusu masuala ya ukimwi katika wilaya hiyo.
Watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga wakifurahia gari lililotolewa msaada na Walter reeds
Alisema kuwa hivi sasa wafadhiri wameanza kupunguza misaada katika maeneo mbalimbali hali ambayo inatoa tahadhari kuwa wananchi wanapaswa kulipa kodi ili tujitegemee badala ya kuwaza ufadhili kutoka kwa wahisani.
- Dkt Chintowa alisema kuwa shirika hilo limekabidhi gari hilo ambalo limetokana na msaada kutoka kwa walipakodi wa Marekani,hivyo nijukumu la wananchi sasa kulipa kodi ambapo serikali itapata fedha na kugharamia miradi yake badala ya kutegemea ufadhili ambao umekua ukipungua siku hadi siku.
Gari aina ya Landcruser iliyotolewa msaada na Walter reeds kwa halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga
Alisema kuwa serikali ya awamu ya tano inajituma sana katika kukusanya mapato hivyo basi hatuna budi kuiunga mkono kwa kulipa kodi kwa wakati ambapo utapata fedha hizo na kugharamia miradi sambamba na kuanzisha miradi mipya kwani huu sasa ni wakati wa kujitegemea.
Naye mganga Mkuu wa mkoa wa Rukwa Bonifas Kasululu alisema kuwa analishukuru shirika hilo kwani zimekuwa ni msaada mkubwa sana na zimekuwa likitoa msaada mingi ambayo zimekuwa ikitumika katika miradi ya ukimwi katika mkoa huo.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Sumbawanga Karolo Ntila akionesha funguo ya gari aliyokabidhiwa na afisa ufundi wa Walter reeds Dkt Chintowa
Alisema kuwa hivi karibuni shirika la Walter reed litaleta mashine maalumu katika mkoa wa Rukwa ambayo itatumika kupima kiwango cha virusi vya ukimwi kwa mtu anayeishi na virusi hivyo ambayo inagharimu shilingi bilioni moja ambayo itasaidia katika kujua kunamafanikio kwa kiasi gani katika mapambano ya dhidi ya virusi hivyo.
Alisema kuwa mashine kama hiyo ipo katika mkoa wa Mbeya ambapo vipimo kutoka mkoani Rukwa hulazimika kupelekwa huko lakini ikiwepo mkoani hapa na kuwekwa katika hospitali ya mkoa ya Sumbawanga itapungiza adha za kusafirisha vipimo mpaka kwenye mkoa wa Mbeya badala yake vitakuwa vikifanyika mkoani humo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga Karolo Ntila alilishukuru shirika hilo kwa msaada huo wa gari na kuwasihi wasichoke kuikumbuka halmashauri hiyo kwa vitendea Kazi pamoja na mafunzo kwa wataalamu ili wananchi waweze kupata huduma bora na za kisasa.
Aidha mwenyekiti huyo alimuagiza kaimu mkurugenzi wa halmashauri hiyo Deogratius Kangu kuhakikisha kuwa halmashauri inaheshimu msaada yote ya wahisani na si kuitumia katika shughuli tofauti na majengo kwani wahisani wanapogundua kuwa vitu walivyotoa vinatumika tofauti na matarajio yao huwa hawapendi.
Alisema kuwa haya yeye binafsi hata kuwa tayari kuona gari hilo likitumika kwa shughuli tofauti na iliyotarajiwa kwani halmashauri inamagari yake na hata kama ni mabovu ni bora wayatengeneze kwanza kuliko kulichukua gari hilo na kulitumia katika shughuli tofauti na lililotolewa.
Hata hivyo Ntila aliwaasa wananchi kuendelea kujitokeza kwaajili ya kupima afya zao ili waweze kupatiwa matibabu kwani serikali inatoa bure dawa za kufubaza Makari ya virusi vya ukimwi hivyo ni jukumu la kila mkazi wa halmashauri hiyo kuchukua hatua na si kusubiri mpaka augue sana.
Mwisho
No comments:
Post a Comment