Na Walter Mguluchuma
Katavi
Madiwani wa Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi kwa kauli moja wametoa tamko la kumpongeza Rais John Magufuli kwa hatua madhubuti anazochukua za kuhakikisha Watanzania wanafaidika na kunufaika na rasilimali zilizopo za nchi yao.
Pongezi hizo za Madiwani wote 21 wanaounda Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Mpanda walizilitoa wakati walipokuwa katika kikao chao cha baraza.
Pongezi hizo za Madiwani wote 21 wanaounda Baraza la
Akitoa tamko la pongezi hizo Meya wa Manispaa hiyo Willy Mbogo alisema Madiwani wote kwa kauli moja wanampongeza sana Rais John Magufuli kwa hatua muhimu na za kijasiri anazochukua za kuhakikisha Watanzania wananufaika na kufaidika na rasilamali walizopatiwa namwenyezi Mungu na wanamuunga mkono kwa asilimia mia moja.
Alisema ujasiri,uthubutu na utayari aliouonesha Rais Magufuli kwa faida ya Watanzania ni wakiwango cha juu kwa binadamu wa kawaida na wanaipongeza pia kamati zote mbili zilizoibua mambo mengi ambayo Watanzania walikuwa hawayafahamu.
Wanashangaa na kulaani vikali kwa mtu yoyote ambaye atatumwa na kuhongwa na Mabeberu ili adhoofishe vita hii ya kiuchumi huyo ni msaliti wa Taifa letu na anapaswa kulaniwa na kuzomewa na Watanzania wote .
Mbogo alieleza kuwa tutambue juhudi hizi za Rais wetu mwisho wake ni faida kubwa kwetu sote Watanzania ,Serikali yetu na Halmashauri zetu kwani Nchi itaongeza mapato yake .
Aliwaomba Wabunge wote waondoe itikadi zao za vyama na wawe pamoja kwenye vita hii na kila wakati kwenye jambo lolote ambalo lenye masilahi kwa Taifa ..
Alifafanua kuwa jambo kama linamaslahi ya Taifa hata kama linasemwa na mtu wa mpinzani liungwe mkono na kama linasemwa na mtu wa chama tawala lenye maslahi ya Taifa basi liungwe mkono na hata wapinzani.
Aidha Madiwani wanawalani vikali sana wale wote ambao wamekuwa wakituibia na kupola mapato ya Watanzania kupitia rasilimali za madini yetu .
Diwani wa Kata ya Makanyagio Haidari Sumry alisema juhudi hizo zinazofanywa na Rais ni mkombozi kwa Halmashauri zote hapa nchini kwani zitaongeza kipato chao .
Naye Diwani wa Viti maalumu Jojina Kisalala aiwataka wanawake wote wamuunge mkono Rais wetu kwa kuibua mambo mengine mengi ambayo bado yamefichika.
Alisema Magufuli ameweka historia kwa kuthibiti rasilimali za Nchi ambazo zilikuwa zikitoroshwa nje ya Nchi na kuikosesha Serikali yetu mapato.
Mwisho
No comments:
Post a Comment