Sunday, 25 June 2017

TFDA yateketeza vitu vyenye thamani ya zaidi ya sh milioni 4

Na Gurian Adolf
Sumbawanga

MAMLAKA ya Chakula na dawa nchini (TFDA) imeendelea na zoezi lake la kuteketeza bidhaa zisizofaa kwa matumizi ya binadamu ambazo zimeingizwa na kuuzwa sokoni kinyume na sheria.
Mkaguzi mwandamizi wa TFDA kanda ya nyanda za juu kusini Yola Hudege alisema hayo jana wakati wa zoezi la kuteketeza wa bidhaa aina ya chakula,  dawa za matumizi ya binadamu na vipodozi vyenye viambata vya sumu zenye thamani ya Sh milioni 4.5 vilivyokamatwa katika msako maalumu uliofanyika mjini hapa.
Alisema msako huo uliofanya na wataalamu wa TFDA wakishirikiana nawatendaji wa idara za afya Halmashauri za Manispaa ya Sumbawanga.
Alisema kwamba baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakifanya makusudi
kwa kuingiza na kuuza sokoni bidhaa ambazo zimekwisha muda wake wa
matumizi na zile zilizopigwa marufuku na ambazo hazijasalijiliwa kwa matumizi ya hapa nchini ili wajipatie kipato wakati wakijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.
Mfamasia wa TFDA Manispaa ya Sumbawanga, Fortunata Kumbakumba alisema
kuwa madhara ya vyakula vilivyoisha muda wa matumizi, pamoja navipodozi vilivyopigwa marufuku nchini kutokana na kutengenezwaviambata vyenye sumu ni pamoja na kuwa chanzo cha maradhi mbalimbalimwilini ikiwa pamoja na saratani ya ngozi, ubongo, ini na figo.
Aliongeza kuwa madhara mengine ni kwa mjamzito ambaye wanaweza kuzaawatoto mwenye utindio wa ubongo, ambapo pia wanawake wapo kwenyehatari ya kuota ndevu na mwanaume matiti.
Mratibu wa TFDA Manispaa hiyo, Ally Lubeba alisema halmashauri hiyoimejipanga kuhakikisha inachukua hatua za makusudi kupambana nawafanyabiashara hao wanaoingiza bidhaa hizo sokoni kwa kuchukua hatua za kisheria ikiwa pamoja na kuwafikisha mahakamani.
Alisema pia imejipanga kukamilifu kuhakikisha kuwa inatoa elimu kwawananchi ili waweze kuzitambua bidhaa feki na zile zilizopigwamarufuku.
Aliongeza kwamba kwa kushirikiana na TFDA wanafanya zoezi la kukamatabidhaa hizo linakuwa endelevu hali ambayo itasaidia kuondoa sokonibidhaa zote ambazo hazijasajiliwa kwa matumizi ya hapa nchinizilizokwisha muda wake na zile zilizopigwa marufuku.
Aidha, kwa mujibu wa sheria namba mbili ya mwaka 2009 Shirika la
Viwango Tanzania (TBS) imebainisha hatua zifuatazo zitakazochukuliwa
pindi inapobainika kuwepo kwa bidhaa hafifu, ambazo ni Kuondoa bidhaa
hafifu zilizopo sokoni, Kufuta leseni za wauzaji, Kuweka utaratibu wa
marejesho na fidia,kuweka taratibu za kuharibu bidhaa duni aukuzirudisha zilikoagizwa, kutoza faini.
Rukwa inatajwa kuwa ni dambo la bidhaa feki, zisizosajiliwa zinazotoka
nje ya nchi na vipodozi vyenye viambata vya sumu ambapo bidhaa hizo
zinatoka nchi za Zambia, Malawi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Mwisho.

No comments:

Post a Comment