Na Walter Mguluchuma
Katavi
Vurugu kubwa zimetokea katika machimbo ya madini ya dhahabu ya Isumamilomo Tarafa ya Nsimbo Wilayani Mpanda baina ya wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu na walinzi wa mgodi wa machimbo hayo na kusababisha kibanda cha ofisi cha kupimia dhahabu na chawalinzi kuchomwa moto na wachimbaji huku polisi wakilazimika kupiga rissi hewani na walinzi wa mgodi kwa lengo la kuwatawanya wachimbaji wenye hasira.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Benedict Mapujila aliwaambia wandishi wa Habari kuwa vurugu hizo zilizodumu kwa takribani saa nzima ambapo zilitokea majira ya saa 2:30 za asubuhi katika machimbo hayo.
Kaimu kamanda alisema kuwa chanzo cha vurugu hizo zilitokana na walinzi wa mgodi huo kumkamata mchimbaji mdogo mmoja wa madini ya dhahabu akiwa na jiwe linalosadikiwa kuwa na dhahabu akiwa na lengo la kulitorosha.
Kaimu Kamanda Mapujila alieleza kuwa baada ya mchimbaji huyo kuwa amekamatwa na walinzi hao inadaiwa walianza kumshambulia kwa kumpiga kitendo kilicho wakasilisha wachimbaji wenzake kwa kile walichodai kuwa imekuwa ni tabia ya walinzi wa mgodi huo kuwapiga wachimbaji wadogo.
Kutokana na hali hiyo kundi kubwa la wachimbaji lilijikusanya na kisha kuvamia banda la walinzi wa mgodi na ofisi ambayo limekuwa likitumika kwa ajiri ya kupimia dhahabu na kuliharibu na kisha kulichoma moto na kuliteketeza kabisa .
Alisema wakati wachimbaji hao wakichoma banda hilo walinzi wa mgodi huo walifyatuwa risasi hewani lakini wachimbaji hao hawakujali waliendelea kuharibu kibanda hicho bila kujali risasi.
Polisi walifika katika eneo hilo baada ya muda si mrefu na waliweza kufanikiwa kutuliza vurugu hizo licha ya kukuta kibanda na ofisi vikiwa vimeharibiwa vibaya na kuteketea kwa moto .
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Generali mstaafu Raphael Muhuga alifika kwenye eneo hilo na kisha alisikiliza kero mbalimbali walizozitowa wachimbaji hao wa madini ya dhahabu .
Baada ya kusikiliza kero hizo za wachimbaji hao wadogo Mkuu wa Mkoa Raphael Muhuga aliwataka wachimbaji hao kufuata tararibu zilizowekwa na serikali.
Alisema kitendo cha wachimbaji kutorosha dhabu bila kupima kunasababisha Serikali kukosa mapato yatokanayo na machimbo hayo ya dhahabu .
Eneo hilo la machimbo ya Isumamilo limekuwa ni maarufu sasa kwa kipindi cha miezi minne sasa kutokana na kuwa zinapatikana dhahabu nyingi na kuna wachimbaji wadogo zaidi ya 6,000 ambao wametoka katika Mikoa mbalimbali hapa nchini na hasa wa Kanda ya ziwa na wafanyabiashara wa kununua dhahabu.
Mwisho
No comments:
Post a Comment