Na Gurian Adolf
Sumbawanga
MTU
mmoja aliyefahamika kwa jina la Pius Luteko(42) mkazi wa kijiji cha
Nankanga A tarafa ya kipeta wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa ameuawa kwa
kitu chenye ncha kali kinachodhaniwa kuwa ni panga baada ya kufumaniwa akifanya mapenzi kwenye pagala na
mke wa mtu.
Tukio
la kuuawa mtu huyo limetokea Juni 5, majira ya saa 11:40 ambapo
watuhumia watatu walimvizia mtu huyo na kufanikiwa kumkuta Luteko na
mwanamke huyo katika pagala na ndipo walipomkata kwa kitu kinachodhaniwa kuwa ni panga kisogoni na
kumsababishia kifo papo hapo.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Rukwa George Kyando alisema kuwa baada ya kufanya
mauaji hayo mmoja kati ya watu waliofanya mauaji alifanikiwa kukimbia na
serikali ya kijiji iliwakamata watuhumiwa wawili akiwamo mume wa
mwanamke huyo na kuwafikisha polisi na wanashikiliwa mpaka hivi sasa.
Aidha
kamanda Kyando alisema kuwa siku ya Juni 6 majira ya 11:45 huko katika
kijiji cha Mpansa, kata ya Mpalamawe,tarafa ya Namanyere, wilaya ya
Nkasi kulitokea ajali ya gari lenye namba za usajili STL 3634
Landcruiser deffender mali ya TASAF Mkoa wa Rukwa.
Gari
hilo lilikuwa likiendeshemwa na dereva Saad Yazid(55) mkazi wa
Sumbawanga, liliacha njia na kupinduka na kusababisha majeruhi kwa James
Kapenulo( 37) Afisa Takwimu katika ofisi ya mkuu wa mkoa huo, Aziza
Kalyatila(38) Afisa Ustawi wa Jamii katika ofisi ya mkuu wa mkoa pamoja
na dereva wa gari hilo ambaye ni mtumishi katika ofisi ya mkuu wa mkoa
pamoja na kusababisha uharibifu wa gari.
Kamanda huyo wa polisi alisema kuwa Chanzo cha gari hilo kupinduka ni kuacha njia kutokana na mwendo kasi wa dereva.
Alisema
Majeruhi hao wapo hospitali ya mkoa Sumbawanga kwa matbabu na mtuhumiwa
amekamtwa ingawa naye ni mmoja wapo kati ya majeruhi atafikishwa
mahakamani pindi atakapopata nafuu.
Katika
tukio la mwisho likilotokea pia Juni 6 majira ya saa 01:00 jioni
huko katika kijiji na kata ya Ulumi tarafa ya Uwimbi Wilaya ya Kalambo
Mkoa wa Rukwa pikipiki yenye namba MC 449 ATE aina ya sunlg Iliyokuwa
ikiendeshwa na Emanuel NtanduMfipa(40) mkazi wa Kazonzya aligongana na
mpanda baiskeli, Aitwaye Aidan Mkata Mfipa(17) Mwanafunzi wa Shule ya
Sekondari Mambwe Mkazi wa Ulumi na kumsababishia majeraha ambapo baada
ya kugongwa alivunjika mkono wa kulia.
Aidha katika ajali hiyo mwendesha bodaboda naye alipata majeraha kifuani na wote wamelazwa katika kituo cha afya Mwimbi.
Chanzo
cha ajali ni mwendokasi wa mwendesha pikipiki ambaye pia ni mmojapo
wapo wa majeruhi na amekamatwa na atafikishwa mahakamani baada ya kupata
nafuu.
No comments:
Post a Comment