Na Walter Mguluchuma
Katavi
MWANAFUNZI wa darasa la sita Shule ya Msingi Kapanga Kata ya Katuma Tarafa ya Mwese Wilaya ya Tanganyika Veronica Lucas (13) amekutwa akiwa amekufa baada ya kubakwa hadi kufa na watu wasio julikana na kisha mwili wake kutupiwa kwenye shimo korongo.
Akitoa taarifa ya tukio hilo Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Benedict Mapujila alisema kuwa tukio hilo la lilitokea juzi majira ya saa kumi na moja na nusu jioni Kijijini humo.
Alisema siku ya tukio hilo Veronica aliondoka nyumbani kwao kama kawaida yake na kwenda shule kwa ajiri ya masomo katika shule ya Msingi aliyokuwa akisoma ya Kapanga.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Mapujila alieleza kuwa marehemu baada ya kuwa amekewenda shuleni hakuweza kurudi tena nyumbani kwao hali ambayo iliwafanya wazazi wake wapate shaka kwani marehemu hakuwa na tabia ya kutorudi nyumbani kwao.
Siku iliyofuata wazazi wake na marehemu walikwenda kufuatilia shuleni na hawakuweza kumkuta hali ambayo ilizidi kuwatia wasiwasi zaidi na waliamua kwenda kutoa taarifa kwenye uongozi wa Kijiji hicho.
Viongozi wa Kijiji pamoja na wananchi wa Kijiji hicho waliamua kuanza kumtafuta mwanafunzi huyo kwenye maeneo mbalimbali ya Kijiji hicho kwa muda wa kutwa nzima pasipo kukata tamaa.
Kaimu Kamanda alisema ndipo ilipofikia saa kumi na moja na nusu za jioni waliweza kuukuta mwili wa Veronica ukiwa umetupwa kwenye shimo la korongo huku akiwa amekufa baada ya kubakwa na watu wasio julkana na sehemu zake za siri zikiwa zimeharibika vibaya .
Alisema chanzo cha kifo cha mwanafunzi huyo kilitokana na kubakwa na kisha kuvuja damu nyingi na kupelekea kifo hicho cha kinyama na cha kikatilli na chakusikitisha pia.
Kaimu Kamanda Mapujila alisema mpaka sasa hakuna mtu wala watu waliokamatwa kuhusiana na tukio hilo na jeshi la Polisi linaendelea na msako wa kuwasaka watu waliohusika na tukio hilo.
Mwili wa marehemu baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kidaktari walikabidhiwa ndugu zake kwaajiri ya mazishi ambayo yalifanyika kijijini hapo siku iliyofuata.
Mwisho
No comments:
Post a Comment