Sumbawanga.
Mwalimu Betson Sanga aliyekuwa akifundisha shule yasekondari Milundikwa iliyopo wilayani Nkasi mkoani Rukwa amefariki dunia baada ya kunywa sumu akiwa katika nyumba moja ya kulala wageni
ya mjini hapa.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, George Kyando alisema jana kwamba Mwalimu huyo alifariki dunia juzi usiku huku akiwa ndani ya chumba chake alichokuwa amepanga akiwa katika nyumba moja ya kulala wageni iliyopo eneo la stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani.
Kyando alisema haikufahamika mara mojo chanzo cha kifo cha mwalimu huyo, lakini aliacha ujumbe usemao " kama nadaiwa deni lolote na mtu
amweleze mkurugenzi ambaye ni mwajiri wake, lakini asilaumiwe chochote juu ya kifo chake".
Inasemekana kwamba siku ya tukio mwalimu huyo alifika katika nyumba hiyo ya kulala wageni na kupanga chumba kwa ajili ya kulala na kisha
alikabidhi funguo na kuondoka kuelekea kusikojulikana.
Taarifa zinadai kuwa ilipofika usiku wa manane alirejea katika nyumba hiyo akiwa amelewa na kuchukua funguo kwa mhudumu kisha kuingia ndani
ya chumba chake kwa ajili ya kulala.
Baada ya muda mhudumu wa nyumba hiyo alisikia sauti ya kukoroma kwa sauti ya juu hali iliyomtia wasiwasi na alipokwenda kumgongea kwa muda
mrefu hakuweza kufungua mlango huo ndipo alipoomba msaada kwa wapangaji wengine ili waweze kumsaidia kuvunja mlango.
Walipoingia ndani ya chumba hicho walimkuta akiwa anatokwa na povu mdomoni hali iliyowalazimu kumkimbiza hospitali ambapo njia alifariki
dunia.
Aidha, kwa mujibu wa maelezo ya Kamanda Kyando uchunguzi wa kitabibu
ulibainisha kuwa mwalimu huyo alijiua kwa kunywa sumu.
Alitoa wito kwa wakazi wa mkoa huo kuacha kuchukua maamuzi ambayo yana
athari kijamii na katika familia badala yake hata kama wanamatatizo ni afadhari kushirikisha watu wengine ili waweze kuwasaidia kuyatatua
matatizo hayo.
Mwisho.

No comments:
Post a Comment