Na Walter Mguluchuma
Katavi
WAFANYABIASHARA wa kijiji cha Itenka Tarafa ya Nsimbo wilayani Mpanda mkoani Katavi wamelazimika kutimua mbio na kuyaacha maduka yao wazi baada ya kundi la Watu watano wanaosadikika kuwa majambazi kuvamia kijiji hicho nakupora mali za wafanyabiashara hao na kisha kutokomea kusikojulikana.
Tukio hilo lilitokea Juni 24 majira ya saa 1:30 za jioni ambapo watu hao walivamia kijiji hicho na kufanikiwa kupora fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 4 baada ya kuwatishia kwa kulipua milipuko ya baruti.
Akitoa taarifa ya tukio hilo Kaimu Kamanda wa polisi Mkoa wa Katavi Benedict Mapujila alisema ma jambazi hao walifika kwenye eneo hilo na kuwavamia katika kijiji hicho na kisha kuanza kulipua baruti hewani hali iliyowafanya wafanyabiashara wa maduka wakimbie na kuwacha maduka yao yakiwa wazi.
Kaimu Kamanda Mapujila alis ema kuwa baaada ya wafanya biashara hao kuwa wamekimbia ndipo majambazi hao walipotumia mwanya huo kuingia ndani ya maduka mawili na kupora kiasi cha shilingi 4,300,000 na kisha kutokomea zao.
Baada ya majambazi hao kukimbia ndipo wananchi wa Kijiji hicho walitoa taarifa kwa jeshi la Polisi juu ya tukio hilo na polisi walifika katika eneo hilo baada ya muda mfupi na walianza msako wa kuwasaka majambazi hao hata hivyo hawakufanikiwa kuwakamata.
Alisema polisi walifanya uchunguzi kwenye eneo la kijiji hicho na hawakuweza kufanikiwa kuokota ganda lolote la lisasi hali iliyo ashiria kuwa majambazi hao hawakuwa na bunduki bali walitumia baruti wakati wakitekeleza tukio hilo.
Kaimu huyo wa kamanda alisema hadi sasa kakuna mtu yoyot e aliye kamatwa kuhusiana na tukio hilo na jeshi la polisi linaende na msako ili kuwakamata watu waliohusika kwenye tukio hilo.
Alieleza kuwa jeshi la polisi limewaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili waweze kuwakamata watu hao na kuwa na tabia ya kutoa taarifa Mara tu uhalifu unapofanyika.
Mwisho
No comments:
Post a Comment