Saturday, 10 June 2017

Miaka 20 jela kwa kunaswa na meno ya tembo

Na Walter Mguluchuma
Katavi
Mahakama ya Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi imemuhukumu kwenda jela miaka 20  Robati  Nakie(44) Mkazi wa  Kijiji  cha  Kanoge  Makazi ya  Wakimbizi ya Katumba baada ya   kukumtia hatiani kwa kosa la kukamatwa na meno ya Tembo  yenye   thamani ya  shilingi milioni 120.
Hukumu  hiyo ilitolewa jana  na  Hakimu  Mkazi  Mfawidhi  wa  Mahakama hiyo Chiganga   Ntengwa  baada ya  kuridhika  na  ushahidi  uliotolewa na  upande wa mashta  uliokuwa na  mashahidi  saba.
  Awali  katika   kesi  hiyo Mwendesha  mashitaka  wa  Serikali  wa  Mkoa wa  Katavi  wa  Mkoa wa  Katavi  Jamira  Mziray  aliiambia   Mahakama  kuwa   mshitakiwa  alitenda kosa  hilo oktoba  21 mwaka  2016 huko  katika   Jijiji  cha Kanoge  Makazi ya  Wakimbizi ya  Katumba.
 Mziray  alidai  kuwa   siku ya  tukio  mashitakiwa  alikamatwa na  Askari wa  Hifadhi ya  Katavi  akiwa  na  meno ya  Tembo   vipande  11  vyenye   thamani ya  shilingi milioni 120   ambavyo alikuwa   amevipakia  kwenye  pikipiki  kwa lengo la kwenda kuviuza.
Aliiambia   Mahakama kuwa   kabla ya   mshitakiwa kukamatwa  Askari wa  Hifadhi ya  Taifa ya  Katavi  walipata  taarifa  za siri kuwa  mshitakiwa Nakie   anamiliki  nyara hizo kinyume  cha   sheria  nyara hizo ndipo walipoanda  mtego na kufanikiwa kumtia mbaroni  mshikiwa  akiwa  na  meno  hayo ya  Tembo.
 Hakimu  Chiganga    Ntengwa kabla ya kusoma  hukumu   aliiambia   Mahakama  kuwa  kutokana  na ushahidi  uliotolewa mahakamani  hapo   na  upande wa  mashitaka  ulikuwa na  mashahidi watano na upande wa utetezi ambao haukuwa  na   shahidi  hata mmoja   mahakama  pasipo kuacha shaka imemtia  hatiani mshitakiwa.
Hivyo   Mahakama kwa kutumia kifungu  cha   sheria   namba 235  cha  kanuni ya  adhabu  na  sheria   ya  wanyama  pori ya  mwaka  2009 imemtia hatiani na kumpeka jela mtuhumiwa huyo.
Hakimu   Chiganga  alitoa  nafasi kwa  mshitakiwa   kama   anayosababu  yoyote ya  msingi ya  kuishawishi   Mahakama  iweze  kumpunguzia  adhabu   ambapo katika   utetezi wake  mshitakiwa  aliiomba   Mahakama  impunguzie   adhabu kwa kuwa    anafamilia   ambayo  inamtegemea, madai ambayo yalipingwa vikali na  mwendesha  mashitaka wa  Serikali   Jamira  Mziray  ambaye alidai kuwa angejua kuwa anategemewa asingejihusisha katika katika suala la kumiliki nyara za serikali na mwendesha mashtaka huyo aliiomba  Mahakama  itoe  adhabu kali  ili  iwe funzo kwa  wengine.
Baada ya  kuzisikiliza  pande  hizo  mbili   Hakimu  Chiganga   alisoma  hukumu hiyo na  kusema Mahakama  imemuhukumu  mshitakiwa kifungo  cha  miaka   20  jela  kuanzia siku ya jana.
Mwisho

No comments:

Post a Comment