Sunday, 11 June 2017

Jela miaka mitatu kwa wizi

Na Israel Mwaisaka
Nkasi
MAHAKAMA ya wilaya Nkasi mkoani Rukwa imemuhukumu kwenda jela miaka mitatu mfanyakazi wa kampuni ya ujenzi wa barabara ya lami ya Kizi-Kanazi ya China Hunan Construction Rashid Chande (36) kwa kosa la wizi la kuiibia kampuni hiyo.
Akisoma hukumu hiyo Juni 9 majira ya saa  6:30 za mchana hukumu  iliyichukua dakika 15,  hakimu mkazi wa mahakama hiyo Ramadhan Rugemalila alidai kuwa mahakama hiyo imeridhishwa na maelezo ya upande wa mashitaka ambao uliitisha mashahidi watatu na kumkuta mtuhumiwa na kosa na nisha  kumtia hatiani.
Awali upande wa mashitaka ukiongozwa na mwendesha mashitaka wa mkaguzi wa polisi Hamimu gwelo ulisema kuwa mtuhumiwa huyo mnamo Disemba 21-2016 aliibia kampuni ya ujenzi anayofanyia kazi kampuni ya China Hunan Construction  kifaa kijulikanacho kama Control box ya Grade namba,PD 003 yenye thamani ya Tshs,Mil.16.
Ilidaiwa kuwa mtuhumiwa huyo  aliiba Box hilo katika kambi ya Wachina lililopo  Namanyere maeneo ya Kipundukala yeye akiwa fundi makenika wa kampuni hiyo na alifanya hivyo huku akijua kuwa hilo ni kosa kisheria.
Upande wa utetezi mshitakiwa alijitetea peke yake na ndipo mahakama ilipomkuta mtuhumiwa na hatia na kumuhukumu kwenda kutumikia kifungo hicho cha miaka mitatu jela.
Hata hivyo mahakama haukuupa uzito utetezi wa mtuhumiwa kwani alidai kuwa anategemewa na familia yake na kwakuzingatia kuwa tabia ya wizi ni kosa kisheria hivyo ikamuamuru akakae jela kwa muda huo ili iwe fundisho pia kwa watu wenye  tabia  za wizi.
Mwisho

No comments:

Post a Comment