Na Gurian Adolf
Katavi
Mahakama ya wilaya ya Mlele mkoani Katavi, imemuhukumu
kifungo cha maisha jela kijana aitwaye Richard Chambanenje (28) mkazi
wa Inyonga kwa kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto wa miaka sita
wakati wakiwa shambani.
Hukumu hiyo imetolewa jana na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo,
Teotimus Swai baada ya mtuhumiwa kukiri kosa mahakamani.
Awali, Mwendesha Mashtaka mkaguzi wa Polisi, Baraka Hongoli alisema
mahakamani hapo kwamba mshitakiwa alitenda kosa hilo Januari 20 mwaka
huu nyakati za saa saba mchana baada ya kuondoka nyumbani na kwenda
shambani kufukuza ngedere.
Mwendesha Mashitaka Hongoli alisema Chambanenje alikuwa akiishi na
kufanya kazi za ndani nyumbani kwa Joseph Felix ambaye ni mzazi wa
mtoto huyo ambapo siku ya tukio aliondoka na mtoto huyo akiwa na
wenzake kwenda shambani kwa lengo la kufukuza ngedere.
Alieleza mahakamani hapo kwamba walipofika shambani mshatikiwa
alimchukua mtoto huyo na kujificha nae katika kichaka cha shamba na
kumbaka hali iliyosababisha mtoto huyo kupiga kelele kutokana kupata
maumivu makali na kuvuja damu katika sehemu zake za siri.
Alisema mshitakiwa alipopelekwa polisi alikiri lakini mahakamani
halikana hivyo upande wa mashataka ulipeleka mashahidi nane lakini
ilipofika jana mshitakiwa aliiomba mahakama asomewe upya shitaka lake
na baada ya kusomewa akiri kutenda kosa hilo.
Mwendesha Mashataka Hongoli aliiomba mahakama itoe adhabu kali ili iwe
fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.
Akitoa adhabu hiyo kwa kuzingatia vifungu vya sheria 130 (1) (2) E na
kifungu cha 131 (3) na kwamba mtoto yupo chini ya miaka 10, Hakimu
Swai alimuukumu kwenda jela maisha.
Mwisho.

No comments:
Post a Comment