Wednesday, 3 May 2017

Usafi wa mazingira bado ni changamoto Manispaa ya Sumbawanga

Gurian  Adolf
Sumbawanga
 
BAADHI ya wakazi wa maeneo ya Jangwani barabara mbili (two ways) mjini Sumbawanga wako katika hatari  ya kukumbwa na magonjwa ya mlipuko ikiwemo ni pamoja na kipindupindu kutokana na kutokuwa na tabia  ya kufanya usafi.

Katika baadhi ya maeneo hayo hali ni mbaya kutokana na kuwa na uchafu mpaka vichichoroni huku katika mitaro ya kupitishia maji hali ndo mbaya zaidi.

rukwakwanza.blogspot ilipata  nafasi ya kuzungumza na wakazi hao walidai kuwa baadhi ya watu wamekuwa hawana  tabia  ya kufanya usafi katika maeneo wanayoishi wakiamini kuwa kazi hiyo ni ya Halmashauri ya Manispaa.

Mmoja wa wakazi hao aliyejitambulisha kwa jina la  Joseph Katanga alisema kuwa wao hawapaswi kusafisha mitaro kwani si Mali yao kwakua mitaro hiyo ni eneo la Manispaa wao jukumu lao ni kusafisha katika maeneo ya nyumba wanazoishi.

Alisema kuwa Halmashauri ya manispaa inapaswa kuajiri watu ama kuingia mkataba na makampuni ili yaweze kufanya usafi lakini si kuwaambia wananchi wakafanye usafi katika mitaro.

"Mitaro ni Mali ya Manispaa hivyo basi mkurugenzi kupitia fedha anazopata anapaswa kuajiri watu ama kuingia mkataba na makampuni ili yasafishe lakini si kutuambia wakazi wa maeneo haya tufanye usafi".. Alisema.

Alisema kuwa wao hawachafui mitaro hiyo ila  ni baadhi ya watu wanaopita ndio wanaotupa taka na nyasi zinaota na kwakua Manispaa haifanyi usafi ndiyo maana hali inakua mbaya.

Naye Maria Samaka alisema kuwa wapo watu ambao hua wanazoa  takataka katika mitaro hiyo lakini kwakua mji  ni mkubwa wasipopita kwa siku mbili na baadhi ya watu si wastaarabu wanatupa taka ndiyo maana inachafuka nataka.

Alitoa wito kwa wakazi wa mji  huo kubadirika ki fikra na kupenda tabia  ya usafi ili mji  wa Sumbawanga uwe  msafi daima na wao waweze kuandoka katika hatari  ya kukumbwa na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment