Na Gurian Adolf
Sumbawanga
JESHI
la polisi mkoani Rukwa linamshikilia askali polisi wake anayefahamika
kwa jina la Prudence Michael kwa kosa la kuendesha gari kwa uzembe na kumgonga mtoto Brighton Apollo(3) na kumsababishia kifo chake.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Rukwa George Kyando alisema kuwa kitendo cha
kumgonga mtoto huyo kilisababishwa na uzembe wa dereva barabarani kwani
anapaswa kuwa makini kwakua barabara inatumika na watu wazima, watoto
na viumbe wengine.
Tukio
hilo lilitokea jana Mei 29 majira ya saa 11 za jioni wakati polisi
huyo akiwa anaendesha gari la jeshi hilo maeneo ya jangwani ambapo
alimgonga mtoto huyo.
Alisema kuwa kufuatia tukio hilo polisi inamshikilia askari huyo na anatarajiwa kufikishwa mahakamani kutokana na tukio hilo.
Aidha
Kamanda Kyando alitoa wito kwa madereva kuwa makini pindi wawapo
barabarani wanaendesha vyombo vya moto ili kuepuka ajali za kugonga ama
kusababisha uharibifu wa Mali kwa kugonga au hata wao wenyewe usalama
wao kwakua ajali inapotokea inasababisha madhara makubwa.
Hata
hivyo alitoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki kufuatia msiba huo na
kuendelea kusisitiza umakini kwa watumia Barabara kwa madereva pamoja na
watembea kwa miguu kwani yeye binafsi na jeshi hilo wanasikitishwa
kutokana na ajali hizo.
Mwisho
Duuuu
ReplyDelete