Sumbawanga
KUTOKANA na kuwepo kwa ugonjwa wa ebola katika nchi Jirani ya Kidemokrasia ya Kongo DRC mkoa wa Rukwa unapaswa kudhibiti watu wananoingia na kutoka katika nchi hiyo kwa kutumia njia za panya ili wasisababishe kuingia nchini virusi vya ugonjwa huo.
Akizungumza na wananchi wa mji wa Kirando wilayani Nkasi mkoani Rukwa mkuu wa mkoa huo Zelote Steven alisema kuwa mpaka sasa hakuna mgonjwa wala dalili isipokuwa ni tahadhari na elimu inaendelea kutolewa kwa wananchi wa mkoa huo ambao baadhi ya maeneo yake yanapakana na nchi ya Kongo ambayo tayari imeripotiwa kuwepo kwa ugonjwa wa Ebola.
Gazeti hili lilifanya jitihada ya kuzungumza na wakazi wa maeneo ambayo ndiyo imekuwa njia za panya ambazo wananchi wa nchi za Tanzania na Demokrasia ya Kongo DRC wamekuwa wakizitumia kuingia na kutoka na iwapo serikali itaziwekea ulinzi madhubuti huenza zikasaidia kukabiliana na tishio la ugonjwa huo kuingia hapa nchini.
Akizungumza na gazeti hili mmoja wakazi wa kijiji cha Kirando Matayo Ntiha aliyataja maeneo ambayo hutumika na wananchi wa nchi hizi mbili kuingia na kutoka kuwa ni maeneo ya kijiji hicho cha Kirando Kalungu Mvuna Namasi Kazovu Kaolongwe Kampemba Utinta Pamoja Na Kabwe.
Alisema kuwa kutokana na historia nzuri ya ujirani mwema, udugu kupendana na kuoana watu kutoka katika nchi hizi mbili wamekuwa wakitembeleana kwa lengo la kusalimiana sambamba na kufanya biashara hali ambayo imezoeleka kutokana na kutokuwa na hila mbaya kutoka upande wowote kwakua wamekuwa wakiishi kama ndugu na wakitambua kuwa wote ni waafrika hivyo wamekuwa wakiishi kwa misingi ya kupendana na kujaliana.
Alisema kuwa wananchi kutoka katika nchi ya Kongo wamekuwa wakiingia humu nchini kwa njia halali na haramu kwalengo la kufanya biashara kutembelea ndugu jamaa na marafiki hali kadharika kutoka nchini kwetu Tanzania na kwenda katika nchi hiyo kwa lengo hilo lakini hali imebadirika kutokana na kuwepo kwa ugonjwa wa Ebola hivyo sasa nivizuri serikali ikachukua hatua kudhibiti uingiaji na utokaji wa wananchi kiholela tofauti na hapo awali.
Ntiha alisema kuwa ni jukumu la serikali kupitia wataalamu mbalimbali kudhibiti hali hii iwapo kunania ya dhati ya kuzuia ugonjwa huo usiweze kuingia hapa nchini na elimu kuendelea kutolewa kwa wananchi ili waache kuwapokea wageni kutoka katika nchi hiyo ili kuepusha kuwepo mgeni ambaye anaweza kuingiza ugonjwa huo katika maeneo yao ambayo pia sehemu kubwa yanatenganishwa na ziwa Tanganyika na wakati mwingine inaweza kuwa ngumu kuwadhibiti watu wanaoingia hapa nchini kwa kulindamipaka ila elimu dhidi ya hatari na adhari za mgonjwa huo ndio inaweza ikawa njia sahihi kwakua wananchi wanaogopa kufa kwa ugonjwa huo.
Hivi karibuni Mkuu wa mkoa huo akiwa pamoja na Mkuu wa wilaya ya Nkasi, Said Mtanda walifanya ziara ya siku tatu kwaajili ya kuzungumza na wananchi wa maeneo hayo kwa lengo la kuwasisitiza kuacha tabia ya kupokea na kuwaficha wageni wanaoingia kinyemela nchini kwani huenda wakasababisha kuingia pia kwa ugonjwa huo ambao ni hatari na unagharimu maisha ya watu kwa kiasi kikubwa.
Hata hivyo viongozi hao waliwaahidi wananchi hao kuwa serikali imekwisha kujipanga kwaajili ya kukabiliana na ugonjwa huo ni wao kuhakikisha wanafuata maelekezo kutoka kwa wataalamu na wapunguze sana kukimbilia katika tiba za jadi kwani mengi ya magonjwa hayatibiki huko isipokuwa sayansi tu kupitia hospitali ndiyo inatoa ufumbuzi wa matatizohayo na ndiyo sababu serikali ya awamu ya tano inatenga bajeti kubwa katika wizara ya afya ili wananchi waweze kuudumiwa kupitia huduma za afya za kisasa.
Mwisho
No comments:
Post a Comment