Friday, 26 May 2017

Nkasi wajipanga kukabiriana na Ebola

Na Israel Mwaisaka
Nkasi

IDARA ya afya wilayani Nkasi imejipanga vyema katika kukabiliana na ugonjwa wa Ebola ambao kwa sasa upo Nchi jirani ya Kongo DRC.

Akitoa taarifa kwenye kikao cha kamati ya afya ya wilaya afisa afya wa wilaya Anselmo Kapandila alimesema wamejiandaa yema katika kukabiliana na ugonjwa huo kwa kuainisha mikakati kadhaa waliyoiweka katika kukabiliana na ugonjwa huo.

Alisema kutokana na mazingira yaliyopo ya muingiliano mkubwa kati ya Watanzania na Wakongo kuna hatari kubwa ya kuupata ugonjwa huo na kuwa sasa kilichopo ni kuhakikisha kuwa ugonjwa huo unakabiliwa ipasavyo ili usiweze kuingia hapa Nchini.

Kapandila amedai kuwa moja ya mkakati mkubwa ni kuandaa mikutano ya kutoa elimu kwa jamii juu ya ugonjwa huo na kuimarisha mfumo wa mawasiliano pale itakapotokea mtu mwenye ugonjwa huo atakapoibuka popote pale wilayani Nkasi.

Mwenyekiti wa kamati hiyo na ambaye pia ni mkuu wa wilaya Nkasi Said Mtanda kwa upande wake aliitaka idara ya afya kuhakikisha kuwa inaitekeleza mipango hiyo ipasavyo ili kuweza kukabiliana na ugonjwa huo ambao ni hatari sana.

Mkuu huyo wa wilaya ameendelea kutoa tahadhari ya ugonjwa huo kwa wakazi wa wilaya Nkasi kupitia mikutano yake mbalimbali ya hadhara.
Mwisho

No comments:

Post a Comment