Gurian Adolf
Sumbawanga
Sumbawanga
WAKAZI wa wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa wameshauriwa
kuitumia fursa ya umeme wa REA uliowafikia hivi karibuni katika shughuli
mbalimbali za kimaendeleo ikiwemo ni pamoja na kuanzisha viwanda
vikubwa na vidogo ili viwasaidie kuongeza ajira na kujikomboa kiuchumi.
Ushauri huo umetolewa jana na mkimbizs mwenge wa uhuru
katika kijiji cha Muze wilayani Sumbawanga wakati akitoa ujumbe wa
mwenge katika kijiji cha Muze kilichopo wilayani humo.
Akizungumza katika viwanja vya stendi katika kijiji cha
Muze mmoja wa wakimbiza mwenge kitaifa Fedrick Ndahani alisema kuwa
bado matumizi ya nishati ya umeme katika maeneo mengi hayajafikiwa
lengo.
Alisema kuwa katika maeneo mengi hapa nchini ikiwemo ni
pamoja na wilaya hiyo wananchi wanatumia umeme kwaajili ya kuwasha
majumbani, saloon, kwenye fridge na matumizi mengine madogomadogo ambayo
hayawafanyi kunufaika vya kutosha na nishati hiyo ya umeme.
Ndahani alisema kuwa iwapo wakazi wa wilaya ya Sumbawanga
watatumia vizuri fursa ya kufikiwa na umeme wa REA wataanzisha viwanda
vikubwa na vidogo ambapo umeme utawawezesha kufanya shughuli zao bila
usumbufu kutokana na kuwepo kwa nishati hiyo ya umeme.
Alisema kuwa wajasilia mali waliopo katika wilaya hiyo
wanapaswa kuboresha bidhaa zao hususani katika suala zima la
kuziandaa,ufungashaji na kuziwekea lebo ili waweze kuziingiza sokoni
zikitambuliwa kuwa zinazalishwa katika wilaya hiyo.
Naye mkuu wa wilaya ya Sumbawanga Dkt Halfan Haule
aliwaambia wakazi wa wilaya hiyo kuhakikisha wanaitunza miradi itakayo
zinduliwa na kuwekewa mawe ya msingi kwani serikaki imeijenga kwa
gharama kubwa na inatokana na kodi zao.
Alisema kuwa nia ya serikali ya tano ni kuwaondolea kero
zinazowakabiri wananchi wa wilaya hiyo ndiyo maana imetekeleza miradi ya
maendeleo na niwajibu wao kuhakikisha kuwa wananufaika na miradi hiyo.
Aidha Dkt Haule aliwashukuru wakazi wa wilaya hiyo
waliojitokeza kwa wingi kuulaki mwenge wa uhuru pamoja na wakimbiza
mwenga kitaifa kwani wanaonesha taswira halisi ya upendo, amani na
mshikamano kwa wakazi wa wilaya hiyo kwani wamejitoa kwa hali na mali
katika kufanikisha mbio za mwenge wa uhuru katika wilaya hiyo.
No comments:
Post a Comment