Wednesday, 12 April 2017
Sumbawanga watakiwa kutumia umeme wa REA kuwekeza viwanda
Gurian Adolf
Sumbawanga
WAKAZI wa wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa wameshauriwa kuitumia fursa ya umeme wa REA uliowafikia hivi karibuni katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo ikiwemo ni pamoja na kuanzisha viwanda vikubwa na vidogo ili viwasaidie kuongeza ajira na kujikomboa kiuchumi.
Ushauri huo umetolewa jana na mkimbizs mwenge wa uhuru katika kijiji cha Muze wilayani Sumbawanga wakati akitoa ujumbe wa mwenge katika kijiji cha Muze kilichopo wilayani humo.
Akizungumza katika viwanja vya stendi katika kijiji cha Muze mmoja wa wakimbiza mwenge kitaifa Fedrick Ndahani alisema kuwa bado matumizi ya nishati ya umeme katika maeneo mengi hayajafikiwa lengo.
Alisema kuwa katika maeneo mengi hapa nchini ikiwemo ni pamoja na wilaya hiyo wananchi wanatumia umeme kwaajili ya kuwasha majumbani, saloon, kwenye fridge na matumizi mengine madogomadogo ambayo hayawafanyi kunufaika vya kutosha na nishati hiyo ya umeme.
Ndahani alisema kuwa iwapo wakazi wa wilaya ya Sumbawanga watatumia vizuri fursa ya kufikiwa na umeme wa REA wataanzisha viwanda vikubwa na vidogo ambapo umeme utawawezesha kufanya shughuli zao bila usumbufu kutokana na kuwepo kwa nishati hiyo ya umeme.
Alisema kuwa wajasilia mali waliopo katika wilaya hiyo wanapaswa kuboresha bidhaa zao hususani katika suala zima la kuziandaa,ufungashaji na kuziwekea lebo ili waweze kuziingiza sokoni zikitambuliwa kuwa zinazalishwa katika wilaya hiyo.
Naye mkuu wa wilaya ya Sumbawanga Dkt Halfan Haule aliwaambia wakazi wa wilaya hiyo kuhakikisha wanaitunza miradi itakayo zinduliwa na kuwekewa mawe ya msingi kwani serikaki imeijenga kwa gharama kubwa na inatokana na kodi zao.
Alisema kuwa nia ya serikali ya tano ni kuwaondolea kero zinazowakabiri wananchi wa wilaya hiyo ndiyo maana imetekeleza miradi ya maendeleo na niwajibu wao kuhakikisha kuwa wananufaika na miradi hiyo.
Aidha Dkt Haule aliwashukuru wakazi wa wilaya hiyo waliojitokeza kwa wingi kuulaki mwenge wa uhuru pamoja na wakimbiza mwenga kitaifa kwani wanaonesha taswira halisi ya upendo, amani na mshikamano kwa wakazi wa wilaya hiyo kwani wamejitoa kwa hali na mali katika kufanikisha mbio za mwenge wa uhuru katika wilaya hiyo. Mwisho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment