Gurian Adolf
Sumbawanga
WAKARA wa vipimo katika mikoa ya Rukwa na Katavi umewatahadharisha
wafanyabiashara mkoani humo kutumia vipimo vinavyotambulika kisheria
vinginevyo watakijuta wakikabiliwa na hukumu ya faini ya hadi shilingi
milioni 100 au kwenda jela miaka mitano ama vyote kwa pamoja.
Akizungumza
na rukwakwanza. Blogspot.com meneja wa vipimo mkoani Rukwa na Katavi
Abinery Nzanga alisema kuwa ni lazima wafanyabiashara wote katika mikoa
hiyo kuhakikisha wanatumia mizani na kueleza kuwa baadhi kuzingatia
uzito na si ukubwa wa magunia ambapo alitolea mfano kwa magunia Mkaa
kg 30, mihogo kg 60, mchele 100 maharage 100, mahindi kg 100mpunga kg
75 na ngano kg 90.
Alisema kutokana na wafanyabiashara
kutokuwa na utamaduni wa kutumia mizani umekuwa ukisababisha kutokuwa na
usawa wakati biashara inapofanyika kwani mara nyingi wakulima wamekuwa
wakidhurumika kwani wafanyabiashara wamekuwa wakipima bidhaa kwa
wakulima kwa kutumia madebe lakini wao wanakwenda kuuza kwa kutumia
mizani.
Nzunga alisema kuwa ili kutenda haki kwa makundi yote ni
lazima kipimo cha mizani ambacho ndicho kinatambuliwa kisheria ndicho
kinapaswa kutumika tofauti na hivyo ni ukiukwaji wa sheria na wao
hawatakubali kuona kundi moja likidhurumika.
Naye Juma Chacha
afisa vipimo wa wakara hiyo amesema kuwa hivi sasa wataendesha
operesheni ili kuwakamata wafanyabiashara wanaokiuka sheria hiyo ili
kukomesha biashara ambayo imekuwa ikifanyika bila kufuata sheria.
Kwaupande
wao wafanyabiashara wa soko la Mandera mjini Sumbawanga walisema kuwa
wao hawana tatizo na matumizi ya mizani kwani wakulima ndiyo wamekuwa
wakigoma kutumia mizani kwakuwa hawajui kuisoma.
Walisema kuwa
wakotayari kufuata matakwa ya sheria kwakuwa ndivyo inavyoelekeza ili
kuepuka mkono wa shelia kwakuwa nao wanachotaka haki itendeke pindi
wanapo fanya biashara zao na kusiwepo wa kupata hasara.
mwisho
No comments:
Post a Comment